STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 6.2.2015

SHIRIKA la ndege la Rwanda linampango wa kuanzisha
safari zake kati ya Zanzibar na Rwanda ikiwa ni njia moja wapo ya kukuza
uhusiano na ushirikiano uliopo sambamba na kuimarisha na kukuza sekta za
biashara na utalii kati ya nchi mbili hizo.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe.
Eugene Kayihura aliyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini
Zanzibar.
Katika maelezo
yake, Balozi Kayihura alimueleza Dk. Shein kuwa tayari Shirika la Ndege la
Rwanda linafanya safari kati ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania
katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Dar-es-Salam hivyo haoni sababu ya kutofanya
safari za kuja Zanzibar.
Alisema kuwa
Shirika hilo lina sababu mbali mbali za kufanya safari zake hapa Zanzibar hasa
ikizingatiwa kuwa Rwanda hivi sasa imo
katika mchakato mkubwa wa kukuza sekta ya utalii na biashara hivyo hatua hiyo
itasaidia kuimarisha sekta hizo.
Balozi Kayihura
alisema kuwa wapo watalii wanaotembelea Rwanda, Uganda na Kenya ambao hutumia
Shirika hilo la ndege kwa safari zao hizo za kitalii, hivyo itakuwa ni jambo la
busara kuunganisha safari hizo na Zanzibar hasa ikizingatiwa kuwa Zanzibar
imepiga hatua kubwa kitalii pamoja na kuwepo vivutio vingi vya kitalii.
Aidha, alisema
kuwa Rwanda ina mambo mengi ya kujifunza na kupanua wigo kutoka Zanzibar
kutokana na mafanikio makubwa yaliopatikana katika sekta ya utalii ambapo pia,
alisisitiza kuwa mbali ya sekta hiyo, sekta ya biashara nayo inaweza kuimarika
pale safari za Shirika hilo zitakapoanza kati ya Rwanda na Zanzibar.
Alieleza kuwa
hivi sasa wafanyabiashara wengi wa nchi za Congo, Garbon na nyenginezo zilizopo
Afrika ya Kati wanataka kuja Zanzibar kwa lengo la kufanya biashara hivyo kuaza
kwa safari za Shirika hilo kutawawezesha kufikia lengo lao.
Sambamba na hayo,
Balozi huyo alieleza kufurahishwa kwake na mafanio yaliopatikana hapa Zanzibar
hasa katika sekta ya Utalii na kupongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Shein katika kufanikisha sekta
hiyo.
Pamoja na hayo,
Balozi huyo wa Rwanda alisema kuwa nchi yake imo katika hatua za kuimarisha
uhusiano na ushirikiano kati yake na Zanzibar hasa katika sekta ya elimu huku akikisisitiza kuwa
Rwanda iko tayari kutoa ushirikiano wake katika suala zima la mafunzo katika mazingira
sambamba na kueleza siri ya mafanikio hayo.
Nae Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alisema kuwa Zanzibar inathamini uhusiano na
ushirikiano uliopo kati ya Rwanda na Zanzibar ambao ni wa muda mrefu.
Dk. Shein alisema
kuwa kuanza kwa safari za Shirika la Ndege la Rwanda hapa Zanzibar kutasaidia
kuimarisha na kukuza sekta hizo za maendeleo huku ikizingatiwa kuwa watu wengi
waliopo Zanzibar na wale wa Rwanda wana hamu ya kutembeleana na kukuza uhusiano
wao lakini kinachowakwanza ni suala zima la usafiri.
Akizungumza
ushirikiano katika sekya ya elimu, Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar imebarikiwa
kuwa na Chuo kikuu chake ambacho ndani yake mna Taasisi ya Lugha za Kigeni
hivyo miongoni mwa lugha zinazofundishwa ni Kiswahili na Kifaransa.
Kutokana na hali
hiyo, itakuwa ni jambo la busara kwa nchi ya Rwanda kuleta vijana wake ili
kujifunza Kiswahili na kwa upande wa Zanzibar kupeleka vijana wake ili waende
kujifunza kifaransa nchini humo hatua ambayo itaimarisha uhusiano na
ushirikiano sambamban na kuweza kubanilishana uzoefu.
Pamoja na hayo,
Dk. Shein alimueleza Balozi Kayihura kuwa kutokana na Rwanda kupiga hatua
katika suala zima la usafi wa mazingira, Zanzibar inampango wa kupanua wigo
kutokana na mafanikio hayo kupitia Baraza lake na Manispaa pamoja na Idara
husika ya Mazingira iliyopo chini ya Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwenda
kujifunza kwa kuona hatua zilizofikiwa na Rwanda na hatimae kupata mafanikio
hayo.
“Lazima tujifunze
kupitia sisi wenyewe kati nchi zetu hizi kwani Rwanda imepiga hatua kubwa sana
katika suala zima la usafi wa mazingira”,alisema Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein
alisisitiza kuwa Zanzibar itaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati
yake na Rwanda.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment