Habari za Punde

Wakamatwa wakibadilisha tarehe bidhaa mbovu

Na Fatma Kassim
JESHI la Polisi kwa kushirikiana na Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi, inawashikilia vijana wawili waliokutwa wakibadilisha tarehe ya matumizi katika  ‘body spray’ aina ya Smart, zilizomaliza muda wake wa matumizi mwaka 2014 zinazomilikiwa na kampuni ya Izmir.

Vijana hao ni Sultan Abdalla Okolo (29) mkaazi wa Fuoni na Siraj Maulid Mkara (29)  wa Mwera  ambao walikamatwa katika mtaa wa Fuoni Maharibiko wakifanya shughuli ya kubadilisha tarehe ya matumizi ambapo jumla ya boksi mbili  tayari walikuwa washazibadilisha muda wa matumuzi.

Mkuu wa biashara na uendeshaji wa bodi hiyo, Abdulazizi Shaib Mohammed, alisema waliwakuta vijana hao wakiwa na zana mbali mbali za kubadilishia muda wa matumizi wa bidhaa hizo ambapo walikutwa wakiwa na tina, pamba, viti vya kusafishia meno, brash, rangi na viwembe.

Alisema ‘body spray’ ambazo zilikuwa zishabadilishwa waliziandika tarehe ya  kumaliza muda  wa matumizi mwaka 2015 na kila boksi ilikuwa na jumla ya chupa 60 ambazo zilikuwa zipelekwemadukani kuuzwa.


Vijana hao wana wanatarajiwa kupelekwa katika vyombo vya sheria kuchukuliwa hatua. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.