Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Oman Balozi Juma Othman akipokea Tunzo ya ushiriki iliyotolewa na Mwakilishi kutoka Manispaa ya Mji wa Muscat ambao ni Waandaaji wa Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni. Tanzania imepeleka zaidi ya Watu 40 kuonesha kazi wanazoifanya za sanaa ikiwemo,Uchongaji,uchoraji na ufumaji wa nguo. Kulia ni Kiongozi wa Msafara huo Khadija Battashy na kushoto ni Msaidizi kiongozi Masha Hussein.
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Oman Juma Othman katikati akiwa kashika Tunzo ya ushiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni nchini Oman waliyopewa kutoka Manispaa ya Mji wa Muscat ambao ndio waandaaji wa Maonesho hayo. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Washiriki kutoka Tanzania Khadija Battashy na kushoto ni Msaidizi kiongozi Masha Hussein na Mkuu wa mambo ya kiufundi wa Msafara Moza Habib. (Picha na Faki Mjaka Oman)
No comments:
Post a Comment