Ali Issa na Miza Othman Maelezo.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema inatarajia kuajiri Madaktari Bingwa na Wazalendo katika Kikosi maalumu cha kuzuia Magendo Zanzibar KMKM ili kukidhi haja ya Madaktari katika hospitali ya KMKM iliyopo Kibweni Mjini Unguja.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za Serikali Haji Omar Kheri katika Baraza la Wawakilishi wakati akijibu Swali la Mwakilishi wa Wawi Salehe Nassor Juma aliyetaka kujua lini Serikali itaajiri Madaktari Bingwa kwa kikosi hicho
Waziri Heri amesema Uajiri huo utafanywa katika Msimu mpya wa Ajira kufuatilia upungufu wa Madaktari waliopo ili kusaidia kupunguza mzigo wa kuhudumia Wagonjwa katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Mnazi mmoja.
Amesema Wataajiri Vijana Wazalendo ambao wamesomea fani husika na Ueledi mkubwa wa kutibu Wananchi Hospitalini hapo ambapo Uajiri huo utakwenda sambamba na Programu ya Wamarekani ambao wamekubali kuisaidia hospitali hiyo kwa kutoa Wataalamu wao.
“Kuna mpango wa kupata madaktari bigwa wawili kutoka marekani ili kuisaidia Hospitali yetu ya KMKM iliyopo kibweni Zanzbar” alisema Waziri Kheri.
Aidha Waziri huyo amesema kuwa watanunua Mashine moja ya Uokozi baada ya ile iliyopo kuharibika ambapo Mashine hiyo itatumika kwa kutilia Gesi vifaa vya uokozi.
Hata hivyo amesema watalazimika kununua Mashine nyingine ili kuziweka katika vituo vya uokozi pale uchumi utakavokuwa unaruhusu kufanya hivyo.
Kikosi maalumu cha KMKM kinatoa huduma za jamii ikiwemo Afya ,katika kambi zake zote ambapo Hospitali ya Kibweni ni hospitali kubwa na yakisasa inayotoa huduma za rufaa ili kusaidiana na hospitali kuu ya Rufaa ya Mnazi mmoja.
No comments:
Post a Comment