Mchoro wa Uwanja Mpya wa Mpira wa kisasa katika viwanja vya Mao Tse Tung, uliowakilishwa na kampuni ya Uchoraji ya Kichina kwa Waziri Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Daid Ali Mbarouk, wazirani ili kuona kama kuna mapungufu ili kufanyiwa marekebisho zaidi kabla ya kuaza kwa ujenzi wake. Kama unavyooonekana pichani.
Ujumbe wa Timu ya Kampuni iliochora Mchoro huo ukitowa maelezo ya uwanja huo kwa Waziri wa Habari Utalii na Michezo Zanzibar.na Viongozi wa Wizara na wa michezo Zanzibar.
Balozi Mdogio wa China Zanzibar Balozi Chen, akizungumza wakati wa kuwasilisha michoro ya Uwanja mpira ya Mao Tse Tung kwa Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Said Ali Mbarouk.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo akizungumza katika mkutano huo na Ujumbe wa China Ukiongozwa na Balozi Mdogo wa China Zanzibar Balozi Chen na Kiongozi wa Kampuni ya Uchoraji wa Mchoro huo ya Architet
of Liaoning Provincial Building Design and Research Institute of Chinda Ndg
Zhang Jian, kulia Naibu Katibu Mkuu Utalii Ndg Issa Mlingoti.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Said Ali Mbarouk, akionesha sehemu za Uwanja huo ambazo zinahitajika kufanyiwa marekebishi wakati wa kuaza kwa ujenzi ili uendane na hali ya viwanja vya Kimataifa, uwanja huo utakuwa na viwanja vyote vya michezo baada ya kufanyiwa marekebisho yake. na wataalamu wa ichoro ya ramani ya uwanja huo.
Jopo la Wataalam wa michoro wakifuatilia mkutano huo wa kuangalia mchoro huo baada ya kuoneshwa Waziri wa Michezo Zanzibar, mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Maelezo Kikwajuni Zanzibar.
Jopo la Mainjinia wa Zanzibar wakifuatilia mchoro huo wakati wa kuwasilishwa na kuangalia
Mtaalamu wa Uchoraji wa Uwanja huo Ndg. Zhang Jian, wa Kampuni ya Architet
of Liaoning Provincial Building Design and Research Institute of Chinda, akitowa maelezo wakati wa mkutano huo wa kuwasilisha kwa mara ya kwanza mchoro huo kwa Waziri kushoto Balozi Mdogo wa China Zanzibar Balozi Chen
Balozi Mdogo wa China Zanzibar Balozi Chen, akizungumza wakati wa mkutano huo akitowa ufafanuzi katika mkutano huo wa kuwasilisha michoro ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa Mao Tse Tung.
Pamoja na maboresho lakini Naona bado hasa hautakuwa Wa kisasa. Hebu huko football pitch wa-design majukwaa ya muundo Wa kisahani yenye mapaa il I wakati Wa mvua na jua watu wastirike vizuri. Hats hi yo hongera.
ReplyDelete