Habari za Punde

Mafunzo ya siku mbili kwa walimu wa somo la uraia Pemba

 MKUU wa taluma kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba, Mkubwa Ahmed Omar, akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waalimu wa somo la uraia kisiwani humo, yalioandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar ‘ZLSC’ na kufanyika ukumbi wa skuli ya maandalizi Madungu mjini Chake chake, kulia ni Mratibu wa kituo hicho Fatma Hemed Khamis na kushoto ni afisa mipango wake Safia Saleh Sultan, (picha na Haji Nassor, Pemba).
 MRATIBU wa kituo huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Hemed Khamis, akiwaonyesha waalimu wa somo la uraia kisiwani humo, katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, wakati akitoa mada juu ya ufafanuzi wa katiba hiyo, kwenye mafunzo yaliondaliwa na ZLSC na kufanyika skuli ya Mandalizi Madungu, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
WAALIMU wa somo la uraia kisiwani Pemba wakimsikiliza afisa mipango wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Safia Salehe Sultan (hayupo pichani), wakati akiwakaribisha waalimu hao kwenye mafunzo ya haki za binadamu yaliondaliwa na ‘ZLSC’ na kufanyika skuli ya Mandalizi Madungu mjini Chake chake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.