Habari za Punde

Ufunguzi wa Maonesho ya Asasi za Kiraia kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zenj

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Zahra Ali Hamad, akizindua maonesho ya Asasi za Kiraia katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, maonesho hayo yamewashirikisha wajasiriamali mbalimbali wa Unguja na Pemba kuonesha bidhaa zao kwa Waheshimiwa wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.  
Mwanakikundi kutowa Micheweni Pemba akitowa maelezo ya Kikundi chao kwa Waziri wa Elimu alipotembelea banda lao 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Zahra Ali Hamad akimsikiliza Mwali Mussa Abdi Khamis akitowa maelezo ya matumizi ya Umeme wa Solar , unavyozalishwa.
Mhe Waziri Zahra Ali Hamad akipata maelezo kutoka kwa kiongozi wa Banda la Tume ya Mipango Zanzibar Ndg. Said Faraj Abdallah , wakati alipotembelea banda hilo.
Wananchi waliofika kutembelea maonesho ya Wajasiriamali wakipata maelezo kutoka kwa Bi Zeudi Mvano Abdilah wa kikundi cha Vijana wa Zanzibar Youth Forum .
Wananchi waliofika katika maonesho ya Wajasiriamali wakipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Kikundi cha Wavuvi cha Kojani Pemba wakati walipotembelea banda hilo linalijihusisha na Uvuvi kisiwani Pemba. 

Mhe Suleiman Hemed akiuliza wakati alipotembelea banda la maonesho la Watu wenye ulemavu Zanzibar, kuhusiana na bidhaa zao wanazozalisha na upatakanaji wa wateja wa bidhaa hizo. 

1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.