Habari za Punde

Yaliojiri Baraza la Wawakilishi Zenj.

 Mwakilishi wa Jimbo la Kitope Mhe Makame Mshimba akichangia wakati wa kikao cha Baraza la Wawakilishi kikiendelea kujadili miswada mbalimbali iliowasilishwa kujadiliwa na Wajumbe wa Baraza.
 Wajumbe wakibadilishana mawazo wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Baraza wakiwa na mmoja wa mswada uliowasilishwa katika kikao hicho. 
 Waziri wa Ardhi, Makaazi Maji na Nishati Mhe Ramadhani Abdallah Shabani akijibu maswali yalioulizwa wakati wa kipindi cha maswali na majibu yaliowasilishwa na Wajumbe wa Baraza katika kikao cha asubuhi.
Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Mhe Saleh Nassor Juma akichangia moja ya mswada uliowasilishwa katika kikao hicho, akiwa na msisitizo akichangia mswada huo. 
             Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia michango ya Wajumbe wa Baraza
                                          Wajumbe wakifuatilia michango kwa makini.

Mhe Jussa Ismail akifurahia mchango ukiwakilishwa na Mhe Saleh Nassor Juma, wakati wa kuchangia mswada uliowakilishwa.
 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho akitoka katika Ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirisha Kikao cha asubuhi cha Baraza la wawakilishi, kwa mapumziko ya mchana.  
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho akitoka katika Ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirisha Kikao cha asubuhi cha Baraza la wawakilishi, kwa mapumziko ya mchana.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitoka ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kulia Mwakilishi wa Bumbwini Mhe Mlinde Mbarouk Juma na Mwakilishi wa Mkwajuni Mbarouk Wadi Mussa.
Waziri wa Kilimo na Misitu Mhe Sira Ubwa Mwamboya na Mwakilishi wa Viti Maalum Mhe Marina Thomas, wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa mkutano.   

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akiwa na Wajumbe wa Baraza nje ya ukumbi wa mkutano wakifurahia jambo, baada ya kikao cha asubuhi kuahirishwa.  
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akibadilishana mawazo na baadhi ya Wajumbe Baraza la Wawakilishi wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.