Habari za Punde

Serikali yatenga hekta 1,363 kwaaajili ya ujenzi wa viwanda Tanga



Na. Johary Kachwamba-MAELEZO, DODOMA

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Maeneo ya EPZ pamoja na Shirika la Maendeleo la TAifa (NDC) imeweka matayarisho na utaratibu wa kuvutia wawekezaji eneo la Tanga.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Janet Mbene alipokuwa akijibu swali la msingi la Mhe. Omari Nundu, Mbunge wa Tanga Mjini.

“tayari Mamlaka ya EPZ imetenga hekta 1,363 katika eneo la Neema mkoani Tanga kwaajili ya ujenzi wa viwanda na uthamini wa mali umekamilika” alisema Mhe. Mbene

Aidha Mhe. Alisema NDC ina eneo la hekta 50 huko Kange Mkoani Tanga ambalo maandalizi ya kuliweka tayari kwaajili ya kuvutia uwekezaji yanaendelea.

Juhudi za kuvutia uwekezaji ili kuanzishwa viwanda vipya zimefanyika pia ambapo kuna viwanda vingi vimeanzishwa ikiwa ni pamoja na Kiwanda cha Maweni cha Saruji, Athi River cha Chokaa, Neelkanth cha chokaa, Tanga Pharmaceutical and Plastics LTd, Peepe Tanzania Ltd, Pemba Flour Mill na vinginevyo. 

“kiwanda cha Saruji cha Tanga na Tanga Fresh ni baadhi ya viwanda vilivyoboreshwa mkoani Tanga ambavyo vinafanya kazi na kuongeza uzalishaji. Kiwanda cha Tanga Dairies Ltd, Tanga kilifufuliwa na sasa kinafanya kazi” alisema Mhe. Mbene

 “Serikali imetambua kuwa tatizo la kiwanda cha mbao linatokana na gharama kubwa ya kupata malighafi kutoka Mufindi, Iringa hadi Tanga. Kutokamilika kwa makabidhiano baina ya mwekezaji na Msajili wa Hazina wa Hati zinazomwezesha mwekezaji kuendelea na kazi kumechelewesha uzalishaji katika kiwanda cha chuma. Wizara inafuatilia kwa karibu masuala hayo” aliongezea Mhe. Mbene

Mazungumzo kati ya Serikali na wamiliki wa viwanda vya Mbao na Chuma yalifanyika na kukubaliana jinsi ya wao kuanza upya kutekeleza wajibu wa kimkakati.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.