“Zanlink ambayo sasa inatumia teknolojia ya FIBER, inapenda kuwatangazia kuwa imeanzisha kifurushi cha huduma ya mtandao katika fiber, ambacho kinaitwa “Home Pack”. Huduma ya kifurushi hiki kinapatikana kwa wateja wanaokaa maeneo ya Stone town, Mlandege, Mbweni, Chukwani, Mazizini, Kiembe Samaki na Mombasa. Maeneo mengine yatafuata karibuni
Kifurushi hiki kinapatikana kwa bei nafuu na ni mahususi kwa watumiaji wa majumbani wa huduma ya mtandao (internet), kina spidi ya 512 kbps muda wa mchana na spidi ya 2 mbps muda wa usiku na wikend. Kwa maelezo zaidi unaombwa ufike ofisi yetu iliyopo mtaa wa Vuga baina ya Sinema ya zamani ya Majestik na ofisi za zamani za SUZA.
Sasa unaweza kujiunga na kufurahia huduma ya uhakika na ya bei nafuu kwenye Fiber.”
No comments:
Post a Comment