Habari za Punde

Mhe Bernard Membe Ahutubia Tamasha la Pasaka Dar.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongea katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka ililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015. Pembeni ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akiwapungia watu waliohudhuria katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba amempongeza Mhe. Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka ililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na Mkewe.



Watu waliohudhuria Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akitoa vyeti vya shukrani kwa vyombo mbali mbali  vya habari vilivyoshiriki kwa miaka kumi na tano katika kulitangaza tamasha la Pasaka.
Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akishirikiana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia) na Mchungaji Mwasota kukata keki. Aanayeshudia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akimlisha keki Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na mkewe.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akimlisha keki Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki. Pembeni anayeshuhudia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara.

Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayefahamika kwa jina la Rebbeca Malope akitoa burudani katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.

Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini, Mchungaji Solly Mahlangu mwanamuziki nguli akiimba na kucheza  katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mwimaji Chritina Shusho akiimba katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015..
Mwimbaji Rose Mhando akiwasha moto wa kamata pindo la Yesu katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.

Wakiimba kwa pamoja...

Msanii wa Sarakasi akitoa burudani katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mwimbaji John Lissu na waimbaji wake wakiimba.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Joshua na vijana wake wakiimba.
Kwaya ya Kijitonyama wakiimba katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Kwaya ya Kijitonyama Upendo Group ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuimba katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Marafiki wakifurahia...
Mtangazaji wa Clouds Radio & TV, Samweli Sasali akiongea na waimbaji wa Kwaya ya Kijitonyama Upendo Group...
Taswira ikitafutwa...
Na Mwandishi Wetu, Dar.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa rai kwa viongozi wa dini zote pamoja serikali kuhimiza vijana waipende dini ili kudumisha amani, utulivu na uadilifu.
Mhe Membe amesema hayo wakati akihubutibi maelefu wa watu waliohudhuria Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba amempongeza Mhe Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka.
Katika Tamasha hilo la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions, ambao ndio waandaji wa Tamasha hilo, wamemtunuku Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika kukuza tasnia ya Sanaa nchini.
Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.
Tuzo zimetolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa michango yao katika kutangaza Tamasha la Pasaka.
Viongozi wa Serikali waliohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Mhe. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naMhe. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Tamasha hilo lilihudhuriwa na viongozi wa kidini wakiwemo, Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly na Mchungaji Mwasota.
Tamasha la Pasaka lilianzishwa rasmi mwaka 2000 na huwashirikisha Waimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini na nje ya nchi ambapo mwaka huu limewashirikisha waimbaji kutoka hapa nchini, Afrika Kusini, Uingereza na Zambia.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda wakifuatilia tamasha.
Mshehereshaji akiendesha Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiondoka pamoja na wageni wake mara baada ya kuhutubia.
Nikiripoti toka Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni Mimi Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog...

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.