MC akisoma ratiba ya sherehe za kukabidhi zawadi kwa Mshindi swa Michezo ya Tamasha la Bonaza lililofanyika Zanzibar Timu ya Ikulu Dar-es-Salaam imeishinda Ikulu Zanzibar wakati wa michezo hiyo iliofanyika Zanzibar mwaka huu.
Ndg Ramadhani Bendera akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha usiku walioandaliwa na wenyeji waio Timu ya Ikulu Zanzibar wakati wa michezo ya Tamasha la Bonaza la Michezo lililofanyika Zanzibar mwaka huu Hafla hiyo imefanyika katika moja ya hoteli ilioko Bububu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Dk. Mwinyihaji akiwahutubia wanamichezo wakati wa hafla ya chakuliwa cha usiku kilichofanyika katika hoteli Zanzibar View Bububu Zanzibar, akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyejiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Wanamichezo wakimsikiliza Waziri Dk Mwinyihaji Makame akiwahutubia katika hafla hiyo ya chakula cha usiku kujumuika nao katika hafla hiyo ya kupongezana na kukabidhiwa zawadi mshindi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Dk Mwinyihaji Makame akiwa na Kombe la Mshindi wa Bonaza hilo la Michezo lililoshirikisha timu za Ikulu Tanzania na Ikulu Zanzibar. Timu ya Ikulu Dar imeshinda ushindi wa jumla katika michezo hiyo na kukabidhiwa Kombe wakati wa Hafla ya chakula cha usiku kilichofanyika katika hoteli ya Bububu nje ya mji wa Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Dk Mwinyihaji Makame akimkabidho Kombe la Mshindi wa Bonaza hilo la Michezo lililoshirikisha timu za Ikulu Tanzania na Ikulu Zanzibar. Ndg Hassan Ekoni, Timu ya Ikula Dar imeshinda ushindi wa jumla katika michezo hiyo na kukabidhiwa Kombe wakati wa Hafla ya chakula cha usiku kilichofanyika katika hoteli ya Bububu nje ya mji wa Zanzibar
Afisa wa Ikulu Dar Ndg Hassan Ekoni akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya Ikulu Dar Ndg.Amos Ndege,
Baadhi ya Washiriki wa michezo mbalimbali wakiwa nac Kombe hilo baada ya kukabidhiwa Makame wakati wa hafla ya kupongezana iliofanyika katika hoteli ya BUububu nje ya mji wa Zanzibar.
Waziri Dk Mwinyihaji Makame akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Bonaza la Michezo ya Pasaka wa timu ya Ikulu Dar-es-Salaam.

No comments:
Post a Comment