Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson (Woodrow Wilson International Centre) tarehe 3 Aprili, 2015 jijini Washington DC nchini Marekani. PICHA NA IKULU
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali
ya awamu ya nne inajivunia mafanikio iliyoyapata tangu kuingia madarakani Mwaka
2005 na kuweka msingi imara wa nchi katika kutekeleza Mkakati wa Maendeleo wa
Mwaka 2025 (Tanzania Development Vision 2025) ambao unalenga
kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 3 Aprili, 2015 jijini Washington DC
wakati akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson (Woodrow
Wilson International Centre.
"Naamini
mrithi wangu atayaendeleza na kujifunza kutokana na mafanikio haya na kuendeleza
kutoka pale tutakapoachia" Rais amesema na
kuongeza kuwa pia anatarajia kuwa Tanzania itakuwa na sera na sheria ya
kusimamia Gesi na mapato yake kwa vile inatarajiwa kuanza kupatikana ifikapo Mwaka
2020. Katika mhadhara huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Mabalozi,
wasomi na viongozi wa taasisi hiyo, Rais Kikwete ameelezea mafanikio na
changamoto katika uongozi wake wa miaka 10 katika elimu, siasa, uchumi na
maendeleo ya jamii.
"Najivunia
kuweza kuendelea kuliweka Taifa katika hali ya Umoja pamoja na changamoto zote,
tumepambana na vitisho pale vilipojitokeza na pia tumetoa mchango mkubwa katika
harakati za kisiasa zilizopelekea vyama viwili kutiliana saini maridhiano na
kupata muafaka Mwaka 2010".
Rais
ameelezea na kuongeza kuwa makubaliano hayo yalipelekea Zanzibar kufanya
uchaguzi kwa amani na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina ya vyama vya
CCM na CUF.
"Natumaini
tutafanya uchaguzi huru, haki na amani
ili niweze kumkabidhi Urais mrithi wangu katika hali ya utulivu"
Rais ameongeza.
............Mwisho............
Imetolewa na;
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Washington DC - Marekani
4 Aprili, 2015.
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Washington DC - Marekani
4 Aprili, 2015.
No comments:
Post a Comment