Na Hassan Khamis, Pemba
MAHAKAMA ya mwanzo Wete chini ya hakimu Abubakar Thabit Suleiman, imemhukumu kulipa faini ya shilingi 30,000 kijana Abdul Abdalla Masoud (19) wa Mtoni Chake Chake kwa kosa la wizi.
Mara baada ya mshtakiwa kutinga kizimbani hakimu Abubakar alimuuliza mwendesha mashtaka Stesheni Sajent wa Polisi Khamis Faki Simai, iwapo mshtakiwa ana kumbukumbu ya makosa ya nyuma na kujibu kuwa hana.
Kabla ya kusomwa kwa hukumu mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliiomba mahakama hiyo isimpe adhabu ya kifungo na badala yake imtoze faini ya kiasi chochote cha fedha kutokana na hali halisi aliyojionea wakati akiwa rumande.
“Mheshimiwa hakimu naiomba mahakama ya tukufu isinipe adhabu ya kifungo kutokana na mimi ni motto mdogo na jengine nilipokua rumande watu wananiendelea kinyume na maumbile”, alidai.
Baada ya utetezi huo hakimu Abubakar amesema mahakama yake haina uthibitisho wa maelezo ya mshtakiwa lakini maneno aliyoyazungumza yamekua yakizungumzwa na vijana wengi wanaoenda magerezani kutumikia vifungo, hivyo mahakama hiyo imezingatia suala hilo.
Alisema pamoja na kua ni kosa lake la kwanza na kuamua mshtakiwa alipe faini ya 30,000.
Awali katika maelezo ya kosa ilidaiwa mahakamani hapo kua April 29, mwaka huu, saa 10:59 jioni eneo la Pandani Wilaya ya Wete, mshtakiwa aliiba mafuta ya taa chupa mbili zenye ujazo wa nusu lita kila moja zikiwa na thamani ya 1,300 mali ya msikiti wa “Mnajaa” wa Masipa Pandani.
Kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu 267 (1) na 274 (1) vya kanuni ya adhabu, sheria namba 6 ya mwaka 2004 sheria ya Serikali ya Mapinnduzi ya Zanzibar.
Wakati huo huo Hamad Said Hamad (22) wa Mzambarau takao Wete amehukumiwa kulipa faini ya shilingi 25,000 na akishindwa atumikie chuo cha mafunzo kwa muda wa wiki 3 kwa kosa la kuendesha vespa bila ya kuvaa helment.
Kufanya hivyo ni kinyume na kifungu cha 130(1) (4) sheria ya usafiri barabarani sheria namba 7 ya mwaka 2003 sheria ya serikali ya Mapinduzi ya Zanziba
Matendo ya kulawitiana magerezani yanaripotiwa na watu wengi. Je! Serikali haioni haja ya kulifanyia utafiti suala hili na kama ikithibishwa ni kweli kulipatia ufumbuzi kulikomesha?
ReplyDelete