Habari za Punde

Balozi Seif akijichanganya na wajasiriamali Dodoma


Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar, balozi Seif Ali Iddi ambaye yupo Dodoma kuhudhuria vikao vya chama, amewatembelea wajasiriamali wanawake wanaouza bidhaa mbali mbali za nguo na vitu vya mapambo mbele ya jengo la Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi lijulikanalo kwa umaarufu kama "white house" mjini Dodoma. 

Mbali na kuwatembelea wajasiriamali hao Balozi Seif pia alinunua bidhaa kadha kutoka kwao. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.