Habari za Punde

Manispa ya Kinondoni Yaendelea Kutekeleza Agizo la Rais JK,la Kuondoa Maji kwenye Makazi ya Watu Tegeta, Bunju na Kunduchi,Kujenga Mifereji ya Kudumu Kupitisha Maji Kuelekea Baharini.

Mkuu wa mkoa wa Dar es slaam,Saidi Meck Sadiki(katikati) akiangalia athari ya maji yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar es slaam akiwa ameambatana na wakazi wa eneo hilo la Kunduchi Ununio.Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na DAWASA inaendelea na zoezi la kuyaondoa maji hayo pamoja na ujenzi wa mfereji mkubwa kuelekea baharini utakaokusanya maji kutoka Bunju na Kunduchi na kuyapeleka bahari ya Hindi.
     Kazi ya ujenzi wa mfereji huo mkubwa wenye urefu wa kilometa 2.1 ikiendelea katika eneo la Kunduchi Ununio.


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki ( katikati ) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Musa Nati wakati akikagua utekelezaji wa zoezi la kuondoa maji katika makazi ya watu eneo la Basihayo Tegeta


 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na baadhi ya viongozi wa Maniapaa ya Kinondoni leo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kata ya Bunju na 
Kunduchi kujionea utekelezaji wa agizo la Rais la kujenga mfereji wa maji kuelekea baharini.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na baadhi ya viongozi wa Maniapaa ya Kinondoni leo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kata ya Bunju na 
Kunduchi kujionea utekelezaji wa agizo la Rais la kujenga mfereji wa maji kuelekea baharini(Picha Aron Msigwa)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.