Habari za Punde

Ligi Kuu ya Zanzibar Malindi Yaibuka Kidedea kwa bao 2--1 Dhidi ya Timu ya Chuoni

Beki wa timu ya Chuoni akiondoa mpira golini kwao wakati wa mchezo wao wa funga dimba la Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa amaan, Timu ya malindi imeshinda 2--1.Ligi Kuu ya Zanzibar inategemewa kufikia tamati siku ya Ijumaa kwa michezo miwili mchana na jioni kwa kukabidhiwa Kombe Bingwa wa ligi hiyo kwa mwaka 2015-2016. 

 Wachezaji wa Malindi wakishangilia bao lao la pili na laushindi dhidi ya timu ya Chuoni ikiwa ni michezo ya lala sala kumalizia Ligi Kuu ya Zanzibar nayotarajiwa kumaliziki Ijumaa hii katika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
 Mchezaji wa timu ya Malindi akiwapita mabeki wa timu ya Chuoni wakati wa mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa amaan. Timu ya Malindi imeshinda 2--1 






Kocha Mkuu wa Timu ya Mafunzo Zanzibar Moroco akiwa na Kocha Mkuu wa timu ya Mbeya City kutoka Nchini Belgium Kocha Pieter Demol, akifuatilia mchezo wa ligi Kuu ya Zanzibar kati ya Malindi na Chuoni kuangalia vipaji vya wachezaji wa Zanzibar kwa ajili ya timu yake kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.