Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na Muelekeo wa Bajeti ya mwaka 2015-2016, imetowa kipaumbele katika Sekta ya Afya Barabara na Elimu, kulia Mhasibu Mkuu wa Serekali Ndg Omar Hassan King na kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Juma Ameir, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Vuga Zanzibar.
Waziri Omar Yussuf akisisitiza jambo wakati wa kutowa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na Muelekeo wa Bajeti ya SMZ kwa mwaka 2015-2016, inayotarajiwa kusomwa katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi cha Bajeti Zanzibar 13-5-2015 saa kumi jioni.
Waziri Omary Yussuf akizungumza na kusisitiza Uchumi wa Taifa Umekuwa kwa kiasi kikubwa.
Waziri wa Fedha akizungumza na kusisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari waliofika wakati akizungumzia muelekeo wa bajeti ya SMZ kwa mwaka wa fedha 2015-2016.
Maofisa wa WEizara ya Fedha wakifuatilia mazungumzo hayo ya Waziri Omar na Waandishi wa habari katka ukumbi wa Wizara ya Fedha Zanzibar wakati akitowa Muelekeo wa Bajeti ya SMZ.
Waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Fedha Zanzibar akizungumzia muelekeo wa Bajeti kwa mwaka huu wa fedha inayotarajiwa kusomwa wiki ijayo katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi cha Bajeti ya mwaka 2015-2016.
Sio barabara tu za watembea na magari, munawasahau wananchi wa chini ambao wanatembea kwa miguu, miundo mbinu ya maji machafu hakuna zaidi ya barabara, halafu hizi barabara zinatengezwa zikiwa na level ya juu, kiasi ambacho kinafunga maji kutoka sehemu ya upande wa pili.
ReplyDeleteTunaiyomba serikali iwe seriously, bora tujue this year budget wizara ya afya tu iboreshwe, basi ni bora, mwaka unaofata iwe elimu, au miundo mbinu, au maji, lakini tuyaone hayo munayo fanya, mpaka sasa hatuoni hayo maendeleo munayo yapa kipao mbele.
Uchumi umekuwa kwa kiasi kikubwa (data?).
ReplyDelete