Na Abdi Suleiman,
PEMBA.
ABIRA 263 waliokuwa
wakisafiri kwa kutumia Meli ya MV Maendeleo, kutoka Kisiwani Pemba kwenda Unguja,
walikwamwa na kushindwa kuondoka majira ya saa mbili za asubuhi, baada ya meli
hiyo kukwama kwenye fungu la mchanga na kusababisha meli hiyo, kushindwa
kuondoka hadi maji kujaa jioni na kuweza kukwamuka.
Meli hiyo ilikumbwa na kizaaza hicho, mara baada ya kupakia
abiria na kuruhusiwa kuondoka bandarini hapo, majira ya Saa 2:00 za asbuhi na
kukumbwa na hali hiyo, wakati ilipokuwa ikipinda kuelekea unguja na kusukumwa
na upepo hadi katika fungu hilo la mchanga.
Baada ya kutokea kwa tukio hilo uongozi wa meli hiyo
walilazimika kufunga kamba kutoka meli iliko umbali ya mita 200 kutoka
bandarini hapo kwa lengo kuivuta meli hiyo ili iweze kutokana na
kushindikana hadi jioni.
Kufuatia hali hiyo uongozi wa meli hiyo, walilazimika kuanza
kuwatafutia abiria waliokuwemo ndani ya meli hiyo huduma muhimu, ikiwemo
kuwapikia chakula cha mchana pamoja na chai ya usiku, ili wananchi kujiona wako
katika hali ya amani.
Akizungumza na waandishi wa habari mbali mbali waliofika katika
bandari ya mkoani, MKuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalaa, alisema
uongozi wa Serikali ya Wilaya tokea asubuhi wako katika eneo la tukiohilo, ili
kuhakikisha wananchi wanakuwa katika hali ya amani na utulivu.
Alisema meli hiyo imekumbwa na mtihani huo, wakati ilipikuwa
ikipinda kutaka kuelekea unguja na kusukumwa na upepo, uliokuwa ukivuma na
kupelewa kwenye fungi la mchana huku maji yakiwa yanatoka.
"Tokea lilipotokea tukio hili tumefika na kuanza kutafuta
njia ya kuwasaidia wananchi waliokuwemo mule, kwa kuwapelekea chakula ili kuona
wakopamoja na viongozi wao"alisema DC Hemedi.
Alisema baada ya maji kujaa meli hiyo, ilikaguliwa na baadae
kuruhusiwa kuondoka kama itakuwa haina tatizo lolote la kiufundi, ili
kuwaondolea hofu wananchi waliokuwemo humo.
Hata hivyo aliwataka ndugu na jamaa wa abiria waliokuwemo ndani
ya meli hiyo, kufahamu kuwa ndugu na jamaa zao wako katika hali ya amani na
tulivu kwa muda wote.
Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu UVCCM Taifa Zanzibar, Shaka
Hamdu Shaka, aliwapa pole wananchi wote waliokuwemo ndani ya meli hiyo, huku
akiwataka kuwa wastahamilivu na wapole.
Shaka aliitaka mamlaka inayohusika na masuala ya bandari
Zanzibar, kuhakikisha wanatambua umuhimu wa bandari ya MKoani na WEte, kwa
kuweka vitu vya kisasa katika bandari hizo ambazo zimekuwa zikiingizia nchi
pato.
Alisema bandari ya Mkoan na wete zote zimetanuka, kutokana na
wafanya biashara wengi kuzitumia bandari hizo kwa kusafirisha mizigo yao,
kutoka Pemba kwenda Unguja na kutoka Unguja kwenda Pemba.
"Kama mamlaka husika zitakuwa makini na zenye kujali hali
za wananchi wao, zinapaswa kutambua umuhimu wa wananchi wao"alisema Shaka.
Hata hivyo alitaka shirika la bandari Zanzibar, kuhakikisha
wanaipatia tagi bandari ya mkoani ili yanapotoke matukio kama hayo kutatuka
mapema, ili wananchi wasiweze kupata tabu kama ilivyotokea kwa meli ya Mv
Maendeleo.
Naye mweneja wa shirika la meli Zanzibar tawi la Pemba, Mariyam
Omar MAssoud, alisema baada ya kutokea hali hiyo walilazimika kuwatafutia
chakula haraka na kuweza kupikia pamoja na mikate kwa ajili ya chai usiku.
Kwa upande wao wananchi waliokuwepo bandarini hapo, wameiyomba Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar hukakikisha bandari ya mkoni wanaipatiwa tagi maalumu,
ili yanapotokea matukio kama hayo Meli kuweza kuvutwa Mara moja.
Meli ya MV Maendelea ilikumbwa na kazia hiyo, mara baada ya
kutaka kupinda na kuchukuliwa na upepo, hali iliyosababisha meli hiyo isubiri
hadi Saa 11:30 jioni kukwamuka na kuruhusiwa kwenda Unguja kwa sababu malimu.
No comments:
Post a Comment