Habari za Punde

Mv Maendeleo Ilivyokwama na kukwamuka bandari ya Mkoani

 MELI ya Mv Maendeleo iyokuwa imepwewa kwenye fungu la mchanga, wakati ilipokuwa ikitaka kuwenda Unguja baada ya kupakia abira na kusubiri hadi maji yalipojaa na kuweza kuondoka, katika bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, watatu kutoka kushoto akiwa na Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka na viongozi wa bandari wakiangalia jinsi gani meli hiyo itavyo ondoka bandarini hapo.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 MKUU wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari, kufuatai tukio la meli ya Mv Maendeleo kukwama katika fungu la mchanga na kushindwa kuondoka asubuhi hadi jioni ndipo ilipofanya safari ya kwenda Unguja.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
 NAIBU katibu Mkuu UVCCM Taifa Zanzibar Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari, juu ya Tukio la kukwama katika fungu Meli ya Mv Maendeleo na kushindwa kuondoka jana asubuhi na kuondoka Jioni yake, baada ya maji kujaa na kuruhusiwa kuondoka.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
GARI la zimamoto likiwa tayari katika bandari ya Mkoani, kwa ajili ya kutoa huduma ya dharura wakati wowote litakapo hitajika, baada ya meli ya Mv Maendeleo kukwama na kushindwa kuondoka bandarini hapo hadi maji yalipojaa jioni huku ikiwa na abiria 263.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

 WANANCHI  mbali mbali wakiangalia Meli ya Mv Maendeleo ikiondoka kisiwani Pemba, baada ya maji kujaa na kukwamuka na kuanza safari ya kuelekea Unguja jana jioni.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
NAIBU katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka, wakati akitoka katoka katika bandari ya mkoani Kisiwani Pemba, baada ya meli ya Mv Maendeleo kukwamuka na kuruhusiwa kuondoka Mkoani na kuelekea Unguja.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.