Mwakilishi viti maalumu wanawake CUF wilaya ya Chake Chake
Mhe: Salma Mohamed Ali, akimkabidhi dawa na vifaa tiba daktari dhamana wa
hospitali ya Chake Chake, dk Yussuf Hamad Idd vyenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni 7.5 vilivyotolewa na mwakilishi wa Jimbo la Chake chake Mhe:
Omar Ali Shehe.
Daktari dhamana
wa hospitali ya Chake Chake Yussuf Hamad Idd, akitoa neno la shukuran kwa
mwakilishi wa viti maalum wanawake wilaya ya Chake Chake na mwakilishi wa Jimbo
la Chake Chake, baadaya kutoa dawa, vifaa tiba
na mashuka kwa ajili ya hospitali hiyo, vyenye thamani ya zaidi ya
shilingi mlioni 8.5.
Mwakilishi wa viti maalumu wanawake CUF wilaya ya Chake Chake
Mhe: Salma Mohamed Ali, akitoa zawadi kwa watoto waliolazwa katika wodi ya
watoto ya hospitali ya Chake Chake, kabla ya mwakilishi huyo kukabidhi dawa,
vifaa tiba na mshuka kwa uongozi wa hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment