Ofisa Muandamizi wa
Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ndg.
Faki Mjaka akizungumza wakati wa hafla
hiyo ya kumuaga Mtaalam wa Mafunzo ya Upigaji Picha kutoka Japan Mr Hiro,
iliotayarishwa na Wanafunzi hao na kumzawadia zawadi mbalimbali wakati wa hafla
hiyo.
Mr. Hiro Mtaalam wa mafunmzo ya Upigaji wa Picha za Mnato
kutoka Shirika la Kujitolea la Japani (JICA) akiwa makini akimsikiliza Ofisa wa Maelezo Zanzibar
akitowa shukrani kwa mkufunzi hiyo, wakati wa hafla iliofanyika katika ukumbi
wa hoteli ya Kipangani Café Nungwi Zanzibar.
Mr.Hiro Matsuda akizungumza na Wanafunzi wake wakati wa hafla ya kumuaga iliofanyika katika Hoteli ya Kipangani Cafe Nungwi Zanzibar, akitowa shukrani kwa wanafunzi hao wakati wate wa mafunzo yake yaliochukua miaka miwili ya masomo
Wanafunzi wa Kozi ya Upigaji Picha wakimsikiliza Mr Hiro
akitowa nasaha zake kwa Wanafunzi wake
baada ya kumuadalia hafla maalum ya
kumuaga iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kipangani Café Nungwi Zanzibar.
Mkufunzi
Mkuu wa Mafunzo ya Upigaji Picha kwa Wafanyakazi wa Idara mbalimbali za
Serikali na Binafsi wakimsikiliza Mr Hiro Matsuda.
Mmoja wa Wanafunzi wa Kozi ya Upigaji wa Picha kutoka Idara
ya Habari Maelezo Zanzibar Bi Fatma, akimkabidhi kasha ikiwa ni zawadi kutoka kwa Wanafunzi wa
Darasa hilo, Mr Hiroi Matsuda amemaliza muda wake Zanzibar baada ya kutowa
mafunzo hayo kwa muda wa miaka miwili.
Mwanafunzi wa Darasa la Mr Hiro Matsuda Ndg Shibli Haji
Shibli akimkabidhi zawadi ya fulana yenye ujumbe Hakuna
Matata Zanzibar, zawadi hizo zimetolewa na Wanafunzi wa Kozi hiyo.
Mwanafunzi wa Darasa la Mr Hiro Matsuda Bi Miza Omar akimkabidhi
zawadi ya Mlango wa Zanzibar zawadi hizo zimetolewa na Wanafunzi wa Kozi hiyo.
Ofisa Muandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar na
Msemaji wa Timu ya Shaba Wazee wa Dago Ndg Faki Mjaka akimkabidhi Mr Hiro
Matsuda, ikiwa ni kumbukumbu yake kutoka katika Uongozi wa timu hiyo, Mr. Hiro
amebuni Nembo ya Timu hiyo ikiwa katika fulana hiyo na inatumiwa na timu hiyo
rasmin kwa sasa.
Wanafunzi wa darasa la Mr Hiro la Upigaji Picha wakiwa katika ufukwe wa nungwi kwa ajili ya kumuaga mwalimu wao baada ya kumaliza mafunzo ya Upigaji wa Picha na Photoshop, yaliochukua miaka miwili .
Wanafunzi wa Kozi ya Upigaji picha na Photoshop wakifulahia
jambo wakiwa katika ufukwe wa Nungwi.
Mr. Hiro katika kapozi katika moja ya jabali la hoteli ya
Nungwi akiwa na Mwanafunzi wake Othman. Wakiwa katika picha ya kumbukumbu.
Brother Othman leo umenikumbusha kumbusho nisilizo lisahau katika maisha yangu ,hawa jamaa wa JICA ,wakati wanafunguwa ofisi yao Zanzibar nilibahatika kujuilishwa na bosi wa offisi hiyo kupitia watalamu waliokuwa wa FAO nikawa na mara nyingi huyo bosi alikuwa hupenda kufika katika shirika nililokuwa nafanya kazi wakati ule kufanyiwa kazi zake hasa za service vyombo vyake kwa bahati wakati ule walikuwa wanatangazia nafasi au mafunzo ya muda mfupi kwa mwenye mapenzi na uwezo wa kwenda kufanya hayo mafuzo kule Japani ,nilimuendea na kumuonesha shahada zangu zangu zote na mafunzo niliyokuwa nimepata hapa zanzibar na Tz kwa ujumla akanipa form nikajaza na akaipeleka kwao nikajibiwa hakuna pingamizi isipokuwa ni lazima nipate kibali toka wizarani kwanza nikamuendea meneja wangu ambae alikuwa ni binadamu mwenye kujuwa maisha na mwenye Roho na imani ya kizanzibari akanipa baruwa nende wizarani nikaenda wizarani kufika pale nikambiwa nimuone katibu mkuu nikaka pale nikamueleza kinachotakiwa ni yeye kukubali kuwa kutowa fursa ile ili niende wao au serekali ya Zanzibar haitotowa hata senti basi alinambia oo sie hapa tuna watu wengi wana elimu zaidi ya yako haitowezekana niliondoka pale moyo umoto na ikaniuma sana ,lakini kama wasemavyo wazee wetu kwa mungu hakuna zito na kila likuepukalo kuna kheri Mmungu akanifungulia milango ambayo sikutegemea na yeye wakati wa Rais Salmini akakubwa na mitihani leo hii nikija Zanzibar namuona njiani akiwa amevaa viyatu rangi tafauti nilipo mueleza mke wangu ambae ni Mmarekani akanambia wewe usifanye aliyo kufanyia yeye na kama unahisi unataka kumsaidia msaidie na mkumbushe kuwa alikuwa katibu wako inatosha hiyo wapo wengi kama yeye leo hii wamekuwa sichochote si lolote
ReplyDelete