STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
26.5.2015
SERIKALI ya Oman imeikabidhi Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar hundi ya T.Shilingi Bilioni 12.3 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya Kiwanda cha
Upigaji chapa zikiwemo mashine za kuchapishia magazeti na vitabu.
Wakati huo huo,
Serikali ya Oman imeikabidhi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nyaraka za gari
10 zilizotolewa msaada na nchi hiyo zikiwemo za viongozi wakuu.
Balozi wa
Oman katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Saoud Ali Mohamed Al Ruqaishi alimkabidhi Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein hundi hiyo pamoja na nyaraka
hizo za gari, makabidhiano yaliofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Mara baada ya
kupokea hundi kwa ajili ya vifaa vya kiwanda hicho cha Upigaji chapa pamoja na nyaraka
za gari hizo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali
Mohamed Shein alitoa pongezi kwa Serikali ya Oman chini ya uongozi wa Sultan
Qabous Bin Said Al Said kwa msaada wake huo kwa Zanzibar.
Dk. Shein alisema
kuwa msaada huo utasaidia kwa kiasi
kikubwa kuiwezesha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kukamilisha nia na malengo
yake ya kuhakikisha inakuwa na kiwanda chake cha kisasa cha Upigaji Chapa
ambacho kitachapisha magazeti na vitabu.
Katika mazungumzo
hayo, ambapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd
alihudhuria, Dk. Shein alisema kuwa msaada huo unaonesha wazi mahusiano na mashirikiano
mazuri na ya muda mrefu pamoja na mapenzi yaliopo kati ya Serikali ya Oman na
ndugu zao wa Zanzibar.
Alisema kuwa
msaada huo ni muendelezo wa misaada kadhaa iliyotolewa na Serikali ya Oman kwa
Zanzibar ikiwemo ujenzi wa Chuo cha Afya kilichopo Mbweni nje kidogo ya mji wa
Zanzibar pamoja na misaada mengineyo ambayo tayari nchi hiyo imeshaitoa.
Aidha, Dk. Shein
alimuhakikishia Balozi huyo kuwa misaada hiyo itatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa na kusisitiza kuwa Zanzibar inathamini sana uhusiano
na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati yake na Oman.
Dk. Shein,
alisema kuwa kwa niaba ya wananchi pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
ametoa shukurani kwa Serikali ya Oman kwa misaada hiyo ukiwemo msaada huo wa
mkubwa wa fedha.
Pamoja na hayo,
Dk. Shein, kwa mara nyengine tena alimtumia salamu kiongozi wa nchi hiyo na
kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kuwa na afya njema yeye pamoja na
wananchi wa nchi hiyo.
Mapema Balozi wa
Oman Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Saoud Ali Mohamed Al Ruqaishi ambaye alifuatana na Balozi Mdogo
wa Oman anayefanyia kazi zake hapa Zanzibar Mhe.Ali Abdulla Al Rashdi alieleza
kuwa Oman itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake kati yake na Zanzibar.
Balozi huyo wa Oman
nchini Tanzania alisema kuwa ni
matumaini makubwa ya Oman kuwa msaada huo wa fedha taslim kwa ajili ya ununuzi
wa vifaa zikiwemo mashine kwa ajili ya Kiwanda cha Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali
utasaidia kwa kiasi kikubwa katika utengenezaji wa magazeti na vitabu hapa
Zanzibar.
Alisema kuwa kiwanda
hicho kitawawezesha wananchi wa Zanzibar kuweza kuwa na kiwanda maalum cha
kuchapisha magazeti pamoja na vitabu.
Pamoja na hayo,
Balozi huyo alieleza kuwa gari hizo kumi zikiwemo za viongozi nazo zitasaidia kwa
kiasi kikubwa katika kuendeleza shughuli za maendeleo hapa nchini.
Balozi huyo vile
vile, alieleza kuwa Kiongozi wa Oman Sultan Qaboos Bin Said Al Said anathamini
uhusiano na mashirikiano yaliopo kati ya Oman na Zanzibar na kuahidi kuwa hatua
hizo zitaendelezwa kwa upande wa wananchi pamoja na Serikali za pande zote
mbili.
Upatikanaji wa
vifaa hivyo kwa ajili ya Kiwanda hicho cha Upigaji chapa kutakiwezesha kiwanda
hicho kuchapisha magazeti pamoja na vitabu mbali mbali hapa Zanzibar.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
aaaaah! waomani mushafuja ,mushafuja, mushafuja sasa hizo pesa watalishwa jku watuadhibu sisi october,
ReplyDeleteKatika mazungumzo hayo, ambapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alihudhuria, Dk. Shein alisema kuwa msaada huo unaonesha wazi mahusiano na mashirikiano mazuri na ya muda mrefu pamoja na mapenzi yaliopo kati ya Serikali ya Oman na ndugu zao wa Zanzibar.
ReplyDelete(Leo imekuwa ndugu zao kwesho mpeni jukwaa Borafya awatukane hao hao)
Nadhani haukuwa wakati muwafaq kutowa msaada huo na naungana na maoni ya mchangiaji alotangulia.Jengine ni kuwa hao ni wale waarabu mnaowasema ovyo kila siku.Kweli baniani mbaya lakini .......
ReplyDeletesasa tuamini kauli ipi ya kuwa "oman watu wazuri na serekali yao" au ile ya wa "oman wabaya" anayo sema borafya na waziri sitta mbona nyie hamueleweki semeni na shida zenu msitukane watu halafu zawadi mnataka na mnatoa pongezi hii sio siasa bali ni mikasa.
ReplyDelete