Na Takdir Ali –Maelezo Zanzibar.
Viongozi wa vyama vya siasa na Dini wametakiwa kuwashajiisha wafuasi
wao kushiriki katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kujikinga na
matatizo mbali mbali yanayoweza kujitokeza ikiwemo kokosa haki zao.
Amesema Daftari la kudumu la wapiga kura lipo kisheria si kwa matakwa
ya kisiasa hivyo viongozi hao wanapaswa kutumia nafasi zao kuwaelimisha wafuasi
wao kushiriki kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura linaloendelea
kuboreshwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Ayub Mohd Mahmoud
wakati alipokuwa akifungua semina ya kutoa elimu ya uandikishaji na uendelezaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa vijana wa Wilaya ya Magharib A na B
hapa Mwera Wilaya ya Magharibi B.
Amewaaleza vijana kuwa mara baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi
vya siasa mwaka 1992,hali ya siasa Zanzibar
haikuwa nzuri lakini juhudi za viongozi walizochukuwa zimepelekea hali hiyo
kutulia, kwa hiyo si vizuri kwa wazee kuwaachia watoto wao au wajukuu zao Zanzibar isiokuwa na
amani na utulivu.
“Tumerithi nchi yetu kutoka kwa wazazi wetu ikiwa katika hali ya amani
na utulivu sivizuri hata kidogo kuwaachia watoto na wajukuu zetu wakiwa katika
nchi isiyokuwa na amani na utulivu,” alisema Ayub.
Aliongeza kuwa vijana kutoyajua yaliyopita na kujua yaliopo hivi sasa yanapelekea kukosa nafasi ya kufikiri
zaidi katika kutoa maamuzi jambo ambalo amesema wanaweza kutoa maamuzi yasiyo
sahihi.
Mapema akitoa maelezo Afisa uandiskishaji wa Daftari la kudumu la
wapiga kura Wilaya ya Magharibi Maalim Khamis Mussa amesema ili kufanikisha Daftari hilo
linaboreka zaidi mashirikiano ya
pamoja ya wadau mbali mbali ikiwemo vyama vya siasa, vyama vya hiari na Wananchi
wenyewe.
Mwalimu Khamis amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa kuna baadhi ya majina ya watu waliofariki ambao majina yao
hayajaondolewa katika Daftari la kudumu na kusema Tume ya Uchaguzi haina uwezo wa
kuwaondoa waliokosa sifa katika daftari hilo bila ya wananchi kuenda kutoa
vielelezo muhimu .
Wakichangia katika semina hiyo washiriki wameiomba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar
kupitia Tume ya Uchaguzi kuandaa mazingira mazuri ya kuwawezesha wananchi
kushiriki katika daftari la kudumu la wapiga kura bila vikwazo vyovyote
sambamba na kuweka wazi kuwa watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao ambao
hawakupatata fursa hiyo muhimu ya kushiriki.
No comments:
Post a Comment