Habari za Punde

Semina ya usambazaji wa matokeo ya sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2012 Morogoro

 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo mafupi wakati wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
 Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Said akitoa maelezo mafupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakati wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro
 Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe akiwahutubia washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro wakifuatilia kwa makini Semina hiyo.
 


kuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe (katikati) akiwa na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu, Zanzibar na baadhi ya washiriki wa Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika leo mjini Morogoro.
( PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

Na Veronica Kazimoto, Morogoro

 
Usambazaji wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 ni muhimu ili kila ngazi ya utawala iweze kuzipata, kuzielewa na kuzitumia takwimu zitokanazo na Sensa hiyo kwa ajili ya kutunga sera, kuandaa na kutathimini utekelezaji wa mipango ya maendeleo pamoja na kufanya maamuzi sahihi.
 
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe wakati akifungua Semina ya siku moja ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyofanyika mjini Morogoro.
 
"Ni matumaini yangu kwamba, ninyi nyote mliokusanyika hapa  mtazitumia vizuri takwimu hizi ili ziwasaidie katika kuweka vipaumbele vya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa mkoa wa Morogoro", amesema Dkt. Rutengwe.
 
Mkuu huyo wa Mkoa amesisistiza kuwa ni wajibu wa kila Ofisa wa Serikali mkoani Morogoro kuhakikisha takwimu zinazotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 zinakuwa msingi wa mipango  ya maendeleo na kuwa kigezo cha kufanya maamuzi katika kuweka mstakabali wa mkoa wa Morogoro.

Nae  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu akitoa maelezo mafupi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, amesema lengo la Semina hiyo ni kuwaelimisha wadau katika ngazi ya Mkoa, Wilaya na Halmashauri juu ya matumizi ya takwimu za Sensa ya Watu ili waweze kuzitumia katika kupanga na kutathmini program mbalimbali za maendeleo katika ngazi husika.
 
"Dumuni lingine la Semina hii ni kuhamasisha matumizi ya takwimu rasmi katika shughuli zetu za kikazi, ili lengo la kutumia takwimu za Sensa kuboresha maisha ya Mtanzania liweze kutimia", amesema Kwesigabo.
 
Kwesigabo amefafanua kua Semina hiyo ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi itasaidia kujua ni maeneo yapi mkoa wa Morogoro umepiga hatua na maeneo ambayo yanapaswa kutiliwa mkazo ili kuweza kufikia malengo ya kitaifa na kimataifa.
 
Jumla ya washiriki mia moja na kumi (110) kutoka ngazi ya Mkoa, Wilaya na Halmashauri zote mkoani Morogoro wameshiriki katika Semina ya Usambazaji wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 kwa lengo la kupata elimu juu ya matumizi ya takwimu zinazotokana na Sensa hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.