Habari za Punde

Wanachama wa ZUPHE Wapata Mafunzo ya Sheria

 Mwenyekiti wa ZUPHE taifaDk.Zaharan Mohamed Nassor, akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wanachama wa chama hicho, yalioandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar, kulia ni Mratibu wa kituo hicho Fatma Khamis Hemed, na kushoto ni wakili wa serikali Mohamed Juma,

Mratibu wa kituo cha huduma za sheria Zanzibar, ZLSC tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed akielezea kazi za kituo hicho kwa wanachama wa chama cha wafanyakazi ‘ZUPHE’ kwenye mafunzo ya siku mbili kwa wanachama hao, juu ya sheria za kazi, yaliofanyika kituoni hapo, katikati ni Mwenyekiti wa ‘ZUPE’ taifa dk Zaharan Mohamed Nassor, na kushoto ni wakili wa serikali Mohamed Juma,
Wanachama wa ZUPHE wakimsikiliza mtoa mada juu ya kanuni ya utumishi wa umma ya mwaka 2014, kwenye mafunzo ya sheria za kazi yalioandaliwa na kituo cha huduma sheria Zanzibar ZLSC na kufanyika Chake chake Pemba 
Mshiriki wa mafunzo ya sheria za kazi ambae ni mwanachama wa ZUPHE, akiuliza swali kwenye mafunzo hayo yalioandaliwa na kituo cha huduma za sheria Zanzibar ZLCS na kufanyika kituoni hapo mjini Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.