Ujenzi wa bara bara unaoendelea Katika Kiwanja cha Watoto Tibirinzi ambao kiko hatuwa za mwisho kukamilika
Baadhi ya Pembea ambazo tayari zimeshafungwa na zinasubiri Umeme kwa majaribio huko katika Kiwanja cha kufurahishia Watoto Tibirinzi Pemba, kiwanja ambacho kinatarajiwa kutowa huduma Sikukuu ya Idi el fitr inayokuja.
Baadhi ya Pembea ambazo tayari zimeshafungwa na zinasubiri Umeme kwa majaribio huko katika Kiwanja cha kufurahishia Watoto Tibirinzi Pemba, kiwanja ambacho kinatarajiwa kutowa huduma Sikukuu ya Idielfitri inayokuja.
na Bakar Mussa- Pemba.
Afisa Mipango , Utekelezaji na Ufuatiliaji
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) , Khalifa Muumin Hilali,
amewahakikishia Wananchi na Watoto kwa ujumla kuwa Watafaidika na matumizi ya
Kiwanja cha Kufurahishia Watoto kilichoko Tibirinzi Kisiwani Pemba, katika
Sikukuu ya Idi el Fitr inayokuja kwa vile Ujenzi wake umeshafikia asilimia 98%.
Akizungumza na mwandishi wa Habari hizi
huko Kiwanjani Tibirinzi nje kidogo ya Mji wa Chake Chake Kisiwani humo,
alisema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika muda mfupi ujao kwa vile Pembea zote
Tano zimeshafungwa na Umeme mkubwa ambao ulikuwa ni kikwazo cha kuzifanyia
majaribio Mashine zilizopo Kiwanjani hapo tayari mafundi wako hatuwa za mwisho
kumaliza kuunga.
Hilali, alieleza kuwa kazi kubwa iliobakia
kwa sasa ni usafishaji wa kiwanja ambao unaendelea na umaliziaji wa Ujenzi wa
Barabara ya Ndani ya Kiwanja ambayo imefikia hatuwa ya umaliziaji ambapo
Mafundi walihakikisha kuwa kabla ya kumi la kwanza kumalizika watakuwa
wameshamaliza kazi hiyo na tayari kwa matumizi.
“Tatizo letu kubwa tulilokuwa nalo ni Umeme
wa Uhakika ( mkubwa ) na tayari mafundi wapo na wameshafunga Transfoma na
mashine nyengine na Waya umeshafika Kiwanjani kutokea Wesha ni kiasi cha
kuunganisha tu kwa majaribio na Pembea iliobakia mafundi wa Kichina wanasubiri
kukamilika kwa uunganishaji wa Umeme wamalize kufunga na kufanya majaribio,”
alisema .
Kwa Upande wa Meneja wa Mfuko huo Pemba,
Rashid Abdalla Moh’d, alisema kuwa kazi iliobakia ni ndogo na ni ukweli Kiwanja
hicho kitatumika kwa Sikukuu ya IdilFitri inayokuja , baada ya watoto kukikosa
kwa muda mkubwa sasa kwa vile ujenzi umefikia hatuwa za mwisho.
Akizungumzia suala la bei ya Kiwanja kwa
mtu atakae ingia , alieleza kuwa ni Tshs 1,000/= kwa Mtu mzima na 500/= kwa mtoto
na hiyo haina utafauti baina ya Unguja na Pemba.
“ Tatizo letu lilikuwa ni Umeme mkubwa kwa
vile hivi Vifaa haviwezi kwenda kwa Umeme mdogo uliokuwepo na tayari mafundi
kutoka Kampuni ya Molel Electrical Contractors Ltd ya Dar-es-Salaam wanamalizia
kuunganisha kutoka Waya unaotoka Wesha hadi humu ndani,” alieleza.
Nae Fundi Umeme kutoka Kampuni hiyo kutoka
Kampuni hiyo, Engineer , Rwegoshora Clavers, aleleza kuwa kazi ya kuingiza
Umeme ndani ya Kiwanja tayari imefikia hatuwa mzuri na tayari wameshafunga
Transfomer kubwa Kiwanjani hapo na tayari wamesha unganisha na Mashine nyengine
za kuendeshea Mashine za Kiwanjani hapo.
“ Wananchi wasiwe na Wasi wasi Shughuli ya
Umeme imekamilika na tunawaahidi Kiwanja watakitumia bila ya Wasiwasi wowote,”
alieleza Engineer huyo.
Watoto wa Kisiwa cha Pemba , wamekosa
kufurahia Sikukuu katika Kiwanja hicho kwa muda mkubwa tokea pale Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii ZSSF , kuamuwa kukifanyia matengenezo makubwa.
No comments:
Post a Comment