Na Mwandishi Wetu Lindi.
MJUMBE wa
Kamati kuu ya CCM na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Kamillius Membe, amesema
Watanzania wanahitaji serikali itakayosimamia Utawala Bora, haki na Uadilifu,
yenye kujali jinsia na kuzingatia dhima ya uwajibikaji.
Amesema ili
kufikia azma hiyo ni jukumu la Chama cha Mapinduzi kuweka miiko ya viongozi ili
kuzuia mianya ya rushwa na kusiisitiza haja ya kuwepo uadilifu miongoni mwa
viongozi.
Membe
amesema hayo leo katika viunga vya CCM
Mkoa wa Lindi, wakati alipotangaza nia ya kugombea kiti cha Urais wa Serikali
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi.
Akizungumzia
vipaumbele vyake iwapo Chama chake kutamteua kugombea nafasi hiyo na kufanikiwa
kuwa Rais, Membe alisema kuna haja kwa badhi ya sheria ikiwemo ile ya kuzuia
rushwa kurekebishwa.
Alisema
Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la rushwa ambapo baadhi watu wakiwemo
viongozi, kujikita katika kupokea rushwa na kufanya ufisadi, jambo linaloharibu
sifa ya nchi.
Alisema
iwapo atachaguliwa kuiongoza Tanzania, suala la Ulinzi n Usalama ni miongoni
mwa mambo makuu yatakayoshughulikiwa na kuonya kuwa hatakuwa na kigugumizi dhidi
ya wahalifu wanaohusika katika mauaji ya Albino,Madawa ya kulevya,ujambazi na
ugaidi.
Alisema
atasimamaia kwa nguvu zote kulinda mipaka ya Tanzaniaili kuwahakikishia maisha
salama wananchi pamoja na kuimarisha vyombo vya Usalama ikiwemo Polisi kwa
kuvipatia vifaa muhimu vya kisasa vyenye uwezo wa kuwakamata wahalifu.
Aidha
alisema ataaendeleza Tunuya taifa kwa kuhkikisha
Muuungano wa Tanzania unadumu na kuainisha kuwa hatakuwa tayari kumvumilia yeyote atakaejaribu kuhatarisha
muuungano huo.
Alisema kuna
baadhi ya Wazanibari wanakebehi Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya 1964, hivyo kuahidi kuwashughulikia, sambamba na kufanya
juhudi za kujenga mazingira bora katika kuimarisha uchumi na maendeleo ya nchi hiyo.
Akigusia juu
ya uimarishaji wa uchumi, Membe alisema atasimamia uanzishaji wa viwanda vidogo
vidogo pamoja na kuyapa uwezo makampuni
binafsi ili hatimae yaweze kutoa jaira kwa vijana.
Alifafanua
kuwa Serikali yake itajenga vituo vya ufundi na
VETA ili vijana waweze kupata maarifa na ufundi katika masuala mbali
mbali na hatimae kuweza kujiajiri.
Katika hatua
nyingine Membe alisema suala la usawa wa kijinsia nalo litapewa kipaumbele, kwa
lengo la kuondoa dhuluma na udhalilishaji dhidi ya akinamama.
Alisema pia
Serikali itanzisha mabenki maalum kwa ajili ya wanawake ili waweze kujiendeleza
kiuchumi na kijamii.
Mapema Waziri
huyo alisema ameamua kujitosa katika kinyanganyiro hicho baada ya kujiridhisha
kuwa ana sifa zote 13 zilizohitajika kwa wagombea.
Alisema
amekuwa mtumishi mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya chama chake na
kufanikiwa kushika nyadhifa mbali mbali ikiwemo za Uwaziri.
Alieleza
kuwa anakusudia kuendeleza umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania kama ilivyoaisiswa na
hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Nae mmoja wa
Mawaziri katika Baraza la kwanza la Mawaziri, Sir George Kahama alimsifia Waziri
Membe na kusema ni mtumishi msafi, mwenye kuchukia rushwa na ufisadi, ambae
katikadi chote cha utumishi wake alijitolea kuwatumikia Watanzania.
Alisema kiongozi
huyo ni mtaalamu katika masuala a usalama na kuanisha kuwa hilo ni jambo muhimu
katika ustawi wa taifa.
Hatua ya
Waziri Membe kutangaza nia ya kugombea kiti cha Urais kupitia CCM, inakifanya
chama hicho ,kufikisha idadi ya wagombea 22 tangu mchakato huo kuanza

No comments:
Post a Comment