WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Zanzibar, Mhe:Mohamed Aboud Mohammed akizungumza na waandikishaji wa Daftari la
wapiga kura, katika kituo cha Wara kilimo Chake Chake Pemba, wakati
alipotembelea vituo mbali mbali kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Zanzibar, Mhe:Mohamed Aboud Mohammed, kionyeshwa idadi ya vituo vya
uandikishaji wa wapiga kura kwa wilaya ya Chake Chake, kutoka kwa Mdhamini wa
ZEC Pemba Ali Mohamed Dadi wakati alipofanya ziara ya kutembelea vituo mbali
mbali kisiwani Pemba.(Picha na Abdi
Suleiman, PEMBA.)
SHEHA wa Shehia ya Mkoroshoni Khamis Iddi Songoro,
akitoa maelezo ya hali halisi ya Uandikishaji wa wapiga kura wapya katika kituo
chake, mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:
Mohammed Aboud Mohammed alipotembelea kituo hicho.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Mkamo wa Pili wa Rais
Zanzibar, Mhe:Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na msimamizi wa kituo cha
uandikishaji wa wapiga kura cha Chachani Makame Hamad Saidi, wakati
alipokitembelea kituo hicho.(Picha na
Abdi Suleiman, PEMBA.)
WANANCHI mbali mbali wakiwa katika foleni,
wakisubiri kujiandikisha katika daftari la wapiga kura wapya, katika kituo cha
Madungu Chake Chake Pemba, kama walivyokutwa na mpigapicha.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MAKARANI wa tume ya Uchaguzi Zanzibar ofisi ya
Pemba, wakimuhudumia mwananchi kwa kumpiga picha ili kupata kitambulisho cha
upigaji kura, kama walivyokuwa wakiwa kazini.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
WAANDISHI wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya
habari Zanzibar, wakizungumza na msimamizi wa kituo cha Uwandikishaji wapiga kura
wapya katika skuli ya Madungu chake Chake, ambaye jinalake halikupatikana mara
moja.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
MDHAMINI wa ZEC Pemba Ali Mohamed Dadi, akimueleza
jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe:Mohammed
Aboud Mohammed wakati alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya uandikishaji
wapiga kura wilaya ya Chake Chake.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment