Na Zainab Atupae, PEMBA
“Tunauza
roho zetu kwa kusaka riziki…. mikono
iende kinywani na midomo iweze kucheza cheza ‘’.
Hayo ni maneno ya wachimbaji wa mawe eneo la Kwareni Vitongoji ndani ya wilaya ya Chakechake .
“Hatuna hila wala uwezo wakutafuta
kazinyengine zakutuwezesha maisha
yetu ambayo hatuna ajira’’ walikua
wanalalamika nilipofika machimboni.
Pamoja na
yote hayo kazi hii ya uchimbaji
wamawe ni hatari wakati mwengine kupoteza viungo na kupoteza maisha pia.
“Najitahidi
tu lakini mawazo telee kichwani na
machozi kunilegalega nikikumbuka
mwenzangu Hamadi Zahor Faki, alivyo weza kukatikiwa na mwamba wa
jiwe na kufariki hapo hapo” alinieleza kwa uchungu Abdalla ‘bati ambae
nikiongozi wa chimbo hilo.
Hao ni baadhi tu ya mamia ya watu, wakati wanapokuwa
wakiendelea na kazi yao ya uchimbaji wa mawe katika eneo hilo kisiwani Pemba , wanapo
pambana na kazi ngumu na yenye kuhitaji ujasiri.
Wengine
huchimba mawe hayo hata kwa kutumia mapango, na kujikata vidole, huku nyundo
nazo zikitawala eneo hilo kwa Kware, ambao palichangamka ni sawa na soko la
Mwanakwerekwe Unguja.
Kubwa ambalo unaweza kulishangaa na kudondokwa na
machozi hasa kwa alie na huruma, ni kuona wapo wanachimba na kuvunja mawe wakikosa
zanabora za kufanyia kazi sambamba na
mbinu bora za kuchimbia mawe .
Kalamu ya makala hii, haikutosheka na jicho la
mbali, ndipo ilipojongea karibu na kumsaka alau mmoja, na kumkatisha kazi ili aweze kuzungumza name.
“Kaka habari…..naam unataka mawe au wewe ni afisa
kutoka Idara ya mazingira…hapana nahitaji kuzugumza na wewe..hapo alikuwa
kijana mmoja akiwa ameroa jasho.
Kw aliavyokuja haamini kwamba sitonunu mawe, licha
ya kunipokea vyema na hasa baada ya kujua alitembelewa na mwandishi wa habari.
Yeye nilimtoa akiwa chini ya mwamba
mkubwa wenye ugumu ambapo mimi
nilisita na kidogo kwenda huko,
lakini kupiga moyo konde niliamuwa
kuvua viatu vyangu vyenye gundi
ambavyo nilizowea kuvivaa kwenda kwenye sehemu kama hizi zenye mwamba.
‘’ Tukiwa katika
kazi hiyi ya uchimbaji wa
mawe na kuyakata miamba ya mawe na
kuilinda miamba hiyo kwa kuweka kifusi kwaajili ya kulinda mporomoko wa aridhi
unaweza ukatokea,’’ walisema wachimbaji hayo.
Mchimbaji huyo, alinieleza kwamba, miamba ya mawe
ndio inayo zuwiya mmongonyoko wa ardhi
lakini wakati wanapo endelea
kuchimba, baadae huchukuwa fusi
linalokatiwa mawe hayo na
kulimwaga .
Abdalah Mohamed
[ Bati] ambae ndie kiongozi wa
kware hiyo ya mawe, yeye binafsi alisema
ajira kwao ni tatizo kubwa, lakini wameweza kujiajiri na kuweza kupata
maendeleo.
Alisema
wachimbaji mwanzo ulikuwa hauna mapato kutokana na mauzo yalikuwa
yakianzia shilingi 5000 kwa gari moja na hadi
sasa ni shilingi 35,000.
Bati alinifahamisha kuwa licha ya kazi ngumu ya
kulitoa jiwe chini ya mwamba hadi juu, kwa ajili ya kuliuza, bado bei ni ndogo,
ingawa wanatarajia kuongeza shilingi 5000 na kufikia shilingi 40,000 kwa
shehena moja ya gari.
‘’Maisha ni
kitenda wiwi……lazima utafute njia ya kikiteguwa na kukipatia ufumbuzi ilikuweza kupata njia ya kupita na weza kuona mwanga ulio
finikia usoni.’’,alisema Abdalah bati.
Kuhusu ukosefu vietendea kazi vya kutosha vya
kuchimbia mawe ambavyo ndio chanzo
kiubwa cha kutafutia maisha alisema, ni
kikwazo kikubwa kwao.
“Tunachimbia kwa kutumia sururu, vipanga,
majembe kwa ajili ya kutolea vifusi na
tindo kwaajili ya kutolea mawe, yote
hayo nguvu ndio jambo la mwanzo’’,alifafanua Bati.
Kwa sasa wanahitaji vifaa vya kisasa ambavyo
wanaamini kama wakipatiwa ndio watafanyaka kazi zao kwa ufanisi, ambapo hapo
ndio serikali nayo iwape nguvu.
Lakini vipi kuhusu uharibufu wa mazingira katika suala kukata miamba yamawe, nilimuuliza sualini hili bati, naye alisema wameweza kujiaandaa vizuru kwa
kupambana kwa kuweka fusi kila sehemu
wanayo kata mawe.
‘’Mbona sisi wenyewe tuwakua wakali kwamba eti
umeshafukua shimo na kutoa mawe kisha uliwache, tunakukamata hadi
ufukie’’,alisema akimaanisha ameshapata taaluma japo kidogo.
Othuman Khamis naye ni mchimbaji katika kware hiyo,
yeye analalamikia kutokuwa na barabara ya uhakika kutoka afisini kwao hadi njia
kuu.
‘’Inawezekana serikali haioni mchango wetu na ndio
maana tumekuwa tukipiga kelele kuhusu ujenzi wa barabara kwa muda mrefu bila ya
mafanikio’’,alilalamika.
Kwao barabara ni tatizo sugu hasa siku za mvua,
ambapo hukosa wateja na wanokuja hununua kwa bei ya chini, maana bado barabara
ni ya udongo.
Lakini
wachimbaji hawa wakaziomba taasisi husika kuwaongeza elimu ya uchimbaji mawe
ili wafanye kazi zao kwa ufanisi.
Wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa mazoea jambo ambalo
wakati mwengine hujihisi kutengwa na asasi za kiraia na hata serikali kuu, kwa
vile hukosa hata kutembelewa na viongozi na kuwapa maelezao.
Lakini sheha wa shehia ya Vitongoji ambako kware
hiyo ndio iliko Salim Ayoub, aliwataka wachimbaji hao kwanza wao kujikusanya
pamoja.
‘’Njia kubwa ya wao kujikwamua na umaskini na hata
kupata elimu waitakayo wahakikisha wanakuwa na ushirika wao ambao sauti zao
zinaweza kufika mbali zaidi’’,alifafanua sheha.
Said Khatibu yeye ndie mkuu wa kware hiyo, yeye
alisema sio busara eneo wanalochimba wachimbaji hao kupelekewa gari la
kuchimbia kwani huwapa hofu vijana hao.
Alisema
kuwepo kwa sehemu hiyo ni muhimu
kwa kwananchi kwa ujumla kwa kuwapatia
kazi mzuri na kuwaingizia mapato kwa ujumla.
Asilimia
kubwa ya wananchi wa Vitongoji wako huko
kware ya binafsi yamawe kwakazi ya uchimbaji
wa mawe , ambayo ndio ajira yao.
Wakaazi hawa
shehia za Vitongoji na wengine hata kutoka Uwandani, wanaona wakati umefika kwa
serikali kuthamini juhudi zao za kujipatia mapato.
Ama kweli mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe,
haya huwezo kuyashuhudia popote kama sio kware ya Vitongoji Wilaya ya
Chakechake mkoa wa kusini Pemba.
No comments:
Post a Comment