Habari za Punde

Serikali yaanza kujenga kituo cha Tiba na Marekebisho ya Tabia waathirika wa madawa ya kulevya

Na Maryam Kidiko – Maelezo 

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesisitiza azma yake ya kujenga Kituo cha Tiba na Marekebisho ya Tabia (Rehabilitation Center) na kwamba tayari kiasi cha Tshs  Bilioni Moja na Millioni 400 zimetumika katika maandalizi ya Ujenzi wa kituo hicho.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wakati akijibu swali la Mwakilishi Wanu Hafidh Ameir katika kikao cha Bajeti kinachoendelea huko Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar

Waziri Ferej amesema kiasi hicho cha Pesa kimetumika kwa ajili ya kukamilisha Msingi na Uwekaji wa Jamvi katika Jengo hilo linalokadiriwa kuwa la Ghorofa mbili.

Amefahamisha kuwa Pesa hizo ziliidhinishwa Katika Kikao cha Bajeti ya Fedha kwa mwaka 2014-2015 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo hicho.

Aidha Waziri Ferej amesema Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ndio Msimamizi Mkuu wa Masuala yote yanayohusu Dawa za Kulenya katika kupambana na kutoa huduma kwa Walengwa waliopata matatizo hayo.

Amesema kwa sasa Nyumba za upatikanaji nafuu (Sober Houses) zinaratibiwa na Tume ya Kitaifa ya kuratibu  na kudhibiti wa Dawa za kulevya chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tume.

Ameleza kuwa Nyumba zinazofunguliwa na Mtu Binafsi au Asasi hutakiwa kuomba ruhusa za kupata kibali kwa Tume kupitia Mratibu ambaye husimamia Shughuli zote za Nyumba kufuatana na Mwongozo uliowekwa na Tume.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo Bihindi Hamad Khamis amesema Wizara hiyo inafahamu kuwepo kwa Darasa la Mchezo wa Judo kwenye Ukumbi wa Mazoezi uliyojegwa hivi karibuni katika Eneo la Uwanja wa Gombani  Pemba.

Amesema kutokana na kufahamu kuwepo kwa Darasa hilo Wizara inandelea kuimarisha Mchezo huo Kisiwani Pemba.

Vile vile amefahamisha kuwa Michezo yote hapa Nchini inaimarishwa na Vyama vinvyohusika na Michezo hiyo ambapo Mchezo wa Judo nao unasimamiwa na Chama cha Judo cha Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.