Habari za Punde

Balozi Seif aomboleza kifo cha Rais mstaafu wa India Bwana Avul Pakir Jainulabdeen Abdul Kalam

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka saini kitabu cha maombolezo katika Ofisi ya Ubalozi mdogo wa India uliopo Migomani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa India Profesa Abdul Kalam Azad kilichotokea Tarehe 27 Julai 2015.
Balozi Seif akimfariji Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana Setandar Kumar mara baada ya kuweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa 11 wa India Profes Abdul Kalam Azad. 


Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi leo ameweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa India Bwana Avul Pakir Jainulabdeen Abdul Kalam kilichotokea Tarehe 27 July 2015 huko shillong Meghalaya Nchini India.

Balozi Seif Ali Iddi ameweka saini kitabu hicho cha Maombolezo hapo katika Ofisi ya Ubalozi Mdogo waJamuhuri ya India uliopo Mtaa wa Migombani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Bwana Avul Pakir Jainulabdeen Abdul Kalam alishika madaraka ya kuiongoza India tarehe 25 July mwaka 2002 hadi Tarehe 25 July mwaka 2007 akiwa Rais wa 11 wa Taifa hilo kubwa Barani Asia.

Marehemu Abdul Kalam Azad amezaliwa mnamo Tarehe 15 October mwaka 1931 ndani ya ukoo maskini akiwa Mtoto wa Nne miongoni mwa Watoto wa Mzee Avul Pakir Jainulabdeen katika Kabila la Tamil.


Kiongozi huyo wa 11 wa Jamuhuri ya India wakati wa Utoto wake alilazimika kufanya kazi ya kusambaza magazeti mitaani wakati akiwa na umri mdogo kabisa akijaribu kusaidia familia yake ya kimaskini kuongeza kipato ili kupunguza ukali wa maisha uliokuwa ukiikabili familia hiyo.

Bwana Abdul Kalam alipata elimu ya msingi katika Skuli ya Ramanathanpuram Schwarts Matriculation akiwa miongoni mwa wanafunzi bora na mwenye juhudi katika masomo yake na kupelekea kuwa mahiri katika masomo ya Hesabu.

Alijiunga na msomo ya sekondari katika chuo cha Saint Joseph na baadaye kujiunga na chuo Kikuu cha Madras kwa masomo ya sayansi na hatimae kufaulu vyema somo la Physics Mwkaka 1854. 

Mwaka 1955 Marehemu Abdul Kalam alijiunga na mafunzo ya Uhandisi wa shughuli za anga katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Madras akiwana ndoto siku moja kuwa askari wa Anga ndoto iliyofifia baadaye baada ya msongo wa mawazo

Alifanikiwa kupata shahada ya Udaktari na kuwa muhadhiri katika vyuo mbali mbali Vikuu Nchini India kabla ya kujiunga katika ulingo wa Kisiasa katika chama cha National Democratic Alliance { NDA }.

Tarehe 10 Juni Mwaka 2002 Chama cha NDA ambacho kilikuwa na nguvu wakati huo kilimteua Bwana Abdul Kalam kugombea nafasi ya Urais dhidi ya vyama vya Samajwadi Party na National Congress Party ambapo baadaye Chama cha Samajwadi Party kikatangaza kumuunga Mkono Bwana Kalam.

“ Nimehemewa! Kila pahala kwenye vyombo vya Habari na mitandao ya Kijamii nimetakiwa nitoe ujumbe. Nikafikiria ujumbe gani nitatoa wakati huu kwa wananchi wa India ? ”. Yalikuwa ni maneno ya Bwana Abdul Kalam baada ya kuteuliwa na Chama chake kugombea nafasi hiyo ya Urais wa India mwaka 2002.

Bwana Abdul Kalam Azad aliyefikisha umri wa Miaka 83 alikuwa akipenda sana kukutana na watoto wa Skuli za Maandalizi kubadilishana mawazo wakati wa uhai wake hata kipindi alipokuwa na maradaka ya Urais.


Mwenyezi Muungu ailaze roho ya Marehemu Profesa Abdul Kalam Azad aliyekuwa Muumini wa Dini ya Kiislamu Mahali Pepa Peponi. Amin.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.