Habari za Punde

CCM Mikoa Minne ya Unguja Yatoa Tamko Kuhusu Edward Lowassa

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wakiwa wamebaada ya kuingia Mwenyekiti wa Kikao hicho Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Mhe Borafya Silima.kwa kuaza kwa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Mhe Borafa Silima akizungumza katika mkutano huo wakati akiufunguwa kwa kuwasilishwa taarifa ya Tamko la Mikoa kuhusiana na aliyekuwa mgombea wa Urais Mhe Edward Lowassa kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Zanzibar.


Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Wanachama wa CCM wakifuatilia mkutano wa taarifa ya Tamko la Mikoa Minne ya Ungja kuhusiana aliyekuwa mgombea wa CCM Edward Lowassa.

Katibu CCM Mkoa wa Mjini Ndg Mohanmmed Omar Nyawanga akisoma Taarifa ya Tamko la Mikoa Minne ya Unguja kuhusiana na aliyekuwa Mgombea wa CCM nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Tanzania Mhe Edward Lowassa kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Afisi kuu ya CCM Zanzibar
Wajumbe wakiwa makini kusikiliza Taarifa ya Mikoa Mnne ya Unguja kuhusiana na aliyekuwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya Urais Mhe Edward Lowassa, na kuelezea msimamo wa CCM kwa mikoa hiyo kuhusiana na suala hilo. 
Waziri Kiongozi Mstaaf Zanzibar na Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Zanzibar akijibu suali lililoulizwa kuhusiana na kuhama kwa aliyekuwa mgombea wa Urais wa CCM Mhe Edward Lowassa, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mwakilishi wa TumbatuMhe Haji Omar Kheri, akijibu swali lililoulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliowajumuisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar
Wajumbe wakifuatilia maelezo ya Taarifa kuhusu Mhe Edward Lowassa kwa Waanchi wakati Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Mhe Borafya Silima akizungumza wakati wa mkutano huo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wakiwa katika mkutano uliotishwa na Mikoa Mnne ya Unguja kuhusu kutoka kwa Mhe Edward Lowassa ambaye alikuwa Mgombea Urais kupitia CCM na kukihama chama hicho kuhamia Chadema.
Picha na OthmanMapara.Blog. zanzinews.com  

1 comment:

  1. Sasa, sijui tumuamini nani kati ya Mhe. Boraafya na Lowassa!

    Sote tunakumbuka kwamba Mhe .Boraafya na Mhe. Machano Othman Said walikua wanamuunga mkono Lowassa na walidiriki hata kuonekana mkoani Arusha wakati wa utiaji nia wa mhe lowassa.

    Mhe Lowassa nae amesema kwamba bado anaungwa mkono na watu wengi ndani ya ccm na wafuasi wake ni imara na watakua tayari kujiunga nae pale muda mwafaka utapowadia.

    Jee mzee wetu Boraafya, unayoyasema yanatoka moyoni au mdomoni tu?.. vyenginevyo utuachie nafasi hiyo tumpe mtu mwingine!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.