Habari za Punde

Balozi Liberata Mulamula Aagwa rasmin Marekani kurudi Tanzania.

 Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja  na baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC walipokwenda kumuaga nyumbani kwake Bethesda Maryland.


                               Safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dulles ikianza.
 Mhe Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Agnes Mutta Mke wa Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Mhe Balozi Liberata Mulamula pamoja na Mkuu wa Utawala Lily Munanka wakibadilishana mawazo pamoja na familia ya Mwambata wa Jeshi.
 Mhe Balozi Liberata Mulamula akiwa pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta pamoja na Mkewe Agnes Mutta.
               Mhe Balozi Liberata Mulamula akitoa  pasi yake ya kusafiria kwaajili ya kujisajili tayari kwa kuondoka.
                        Mhe Balozi Liberata Mulamula  akiwa katika hatua za mwisho za usajili.
                           Mhe Balozi Liberata Mulamula tayari usajili ulipokamilika
Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi pamoja na familia zao.
Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula akiwa tayari anajiandaa kwa ukaguzi wa mwisho na kuelekea kwenye ndege.
 Kwa pamoja tunasema Safari Njema na Ubarikiwe Sana Balozi Mulamula daima tutakukumbuka.
                    PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI.

1 comment:

  1. Du! yaani tukisema tunaambiwa kuna dalili za kibaguzi lakini ukweli usio pingika katika balozi za Tanzania waZanzibar kidogo sana au hakuna kabisa.

    Wanabaguana au wanatubaguwa lakini naamini kabisa hapa katika hizi picha hakuna hata Mzanzibari mmoja, yaani tuseme wazanzibari ndio hatuna elimu au hatuwezi majukumu ya kazi......
    Hii mifano ipo mengi sana kuanzia wizara ambazo zipo katika muungano na n.k ukiuliza utaambiwa yupo Mh Bi Saada mkuya waziri wa fedha.
    Benku kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar kuanzia Meneja hadi karani wadogo kutoka Tanganyika ndio maana wapinzani wana sera ya ''Haki sawa kwa woote''
    Kumalizia napenda kuwakumbusha kuwa Wazanzibari tunaweza mfano ulio hai Zanzibar insuarance na Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ)zinafanya uzuri katika soko.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.