Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe,Vicente Mebunia Veloso alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe,Vicente Mebunia Veloso alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe,Vicente Mebunia Veloso baada ya mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,([Picha na Ikulu.]
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
3.8.2015

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Msumbiji na Tanzania ni nchi
zenye historia katika uhusiano na ushirikiano wao hivyo kuna kila sababu ya kuendelezwa
na kuimarishwa kwa manufaa ya pande mbili hizo.
Dk. Shein aliyasema
hayo leo wakati wa mazungumzo kati yake na Balozi wa Msumbiji katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania anaemaliza muda wake wa kazi hapa nchini Mhe. Vicent
Mebunia Veloso, yaliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kuaga.
Katika mazungumzo
hayo, Dk. Shein alisema kuwa uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na
Msumbuji ni wa kihistoria hivyo hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika
mashirikiano katika sekta kadhaa za maendeleo ni muhimu na zinamsingi kwa nchi
zote mbili.
Dk.Shein alisema
kuwa Tanzania ikiwemo Zanzibar zina uhusiano na ushirikiano wa kihistoria na Msumbiji
ambao umepelekea wananchi wake kuishi kama ndugu kwa miaka mingi sambamba na
juhudi zinazochukuliwa na serikali za nchi hizo katika kuendeleza hatua hiyo.
Aidha, Dk. Shein
alisema kuwa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inathamini sana uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Msumbiji na kueleza
kuwa mashirikiano yanayoendelezwa yatasaidia katika uimarishwaji wa sekta za
maendeleo zikiwemo elimu, kilimo, gesi na mafuta, utalii na nyenginezo.
Akizungumzia kwa
upande wa sekta ya elimu, Dk. Shen alisema kuwa hatua za ushirikiano uliopo
hivi sasa katika sekta hiyo kati ya Msumbiji na Tanzania umeweza kuleta
mafanikio mazuri na kusisitiza haja ya kuendelezwa kwa upande wa Zanzibar
kupitia SUZA kwani tayari chuo hicho kinafundisha lugha kadhaa ikiwemo
Kiswahili, Kireno,Kichina,
Dk. Shein
alimpongeza balozi huyo kwa mashirikiano mazuri aliyoyatoa katika muda wake
wote aliofanya kazi hapa nchini sambamba na kueleza kuwa ujio wa Rais Filipe
Nyusi hivi karibuni hapa nchini
umeonesha wazi uhusiano na ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Msumbuji
pamoja na kuweko kwa makubaliano kadhaa ambayo yataimarisha uhusiano huo.
Nae Balozi wa
Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Vicent Mebunia Veloso
alitoa pongezi kwa wananchi na viongozi wa Tanzania kwa kumpa mashirikiano
mazuri wakati akiwa nchini akitekeleza majukumu yake ya Ubalozi wa nchi yake.
Balozi Veloso
alisema kuwa Msumbiji inajivunia uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na
Tanzania ambao ni wa muda mrefu hali ambayo imepelekea kuwepo kwa makubaliano
kadhaa katika sekta za maendeleo ambayo baadhi yake yameshaanza kutekelezwa na
kufanyiwa kazi.
Katika maelezoa
yake Balozi huyo wa Msumbiji alisema kuwa
makubaliano yaliofikiwa katika ujio wa Rais Filipe Nyusi pamoja na yale
aliyoyarisi kutoka kwa Rais aliemaliza muda wake Mhe. Armando Guebuza pamoja na
viongozi wa Tanzania yanaweza kuimarisha zaidi uhusiano wa kimaendeleo kwa nchi
mbili hizo.
Aidha, Balozi
huiyo alimuhakikishia Rais Dk. Shein kuwa nchi yake itaendeleza uhusiano na
ushirikiano uliopo ambao unahistoria na hivi sasa tayari matunda yake
yanaonekana hasa katika sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.
Katika mazungumzo
yao viongozi hao pia, waligusia haja ya kukuza uhusiano na ushirikiano katika
sekta ya usafiri na usafirishaji hatua ambayo itarahisisha safari za anga na
bahari kati ya Msumbuji na Zanzibar.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment