Habari za Punde

Matokeo ya Kura ya Maoni CCM Ubunge na Uwakilishi Kwahani Unguja.

Katibu wa CCM Wilaya ya Mjini Fatma Shomari akitaja matokeo ya Jimbo la Kwahani kukamilisha majimbo ya Uchaguzi katika Wilaya yake kukamilika kufanya uchaguzi wa Kura za maoni  baada ya kutoa matokeo ya Majimbo ya Rahaleo, Jangombe na Malindi kubakia Jimbo hilo la Kwahani kutopata matokeo yake wakati wa kutaja majimbo hayo. 

Jimbo la Kwahani kwa Wabunge.tovyo
Kwa nafasi ya Mbunge waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ni Wanachama Wawili nao ni aliyekuwa Mbunge wa Zamani  Mhe Hussein Ali Hassan Mwinyi  na Ndg Jaffar Khamis Ramadhani ndio waliojitokeza katika nafasi hiyo.
Kwa nafasi ya Ubunge mshindi ni Mhe Hussein Ali Hassan Mwinyi kwa kupata kura 3098 kwa kumshinda mpizani wake Jaffar Khamis Ramadhani kwa kupata kura 98.

Kwa Upande wa nafasi ya Uwakilishi Wanachama wa CCM waliojitokeza kugombea nafasi hiwa walikuwa 7.


Mshindi wa nafasi ya kwanza aliyekuwa Mwakilishi wa Zamani wa Jimbo hilo Mhe. Ali Salum Haji.

 Nafasi ya Pili katika kura hizo za maoni imechukuliwa na Ndg Nassor Shaban Ameir kwa kupata kura 671. 

Nafasi ya Tatu imechukuliwa na Ndg. Machano Mwadin Omar kwa kupata kura 642, Kwa 
Nafasi ya Nne imeshikwa n a Ndg Mmaka Hamad Hilika kwa kupata kura 508, 
Nafasi ya Tano imeshikwa na Ndg Abdalla Mohammed Abdalla kwa kupata kura 165. 
Nafasi ya Sita imechukuliwa na Ndg Ameir Juma Othman  kwa kupata kura 99,na 
Nafasi ya Saba imeshikwa na Ndg Hassan Ibrahim Suleiman kwa kura 92.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.