Na Mwinyimvua Nzukwi
Klabu ya waandishi wa habari Zanzibar leo inatarajia kufanya mkutano wake mkuu utakaoambatana na uchaguzi mkuu wa viongozi wa klabu hiyo kuhitimisha kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa sasa.
Katibu mkuu wa klabu hiyo Suzan Peter Kunambi alisem awakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika ofisi za klabu hiyo ziliopo katika jengo la makao makuu ya shirika la posta Tanzania ofisi ya Zanzibar Kijangwani, kuwa mkutano huo utafunguliwa na meneja wa taasisi bima ya maisha ya Afrika (African Life Insurance) tawi la Zanzibar Aisha Reuben Makorongo.
Alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na kwamba jumla ya wanachama 16 wamejitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi wa klabu hiyo utakaodumu kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Alisema wanachama hao ambao ni watendaji kutoka katika vyombo mbali mbali vya habari vya ndani nan je ya Zanzibar wamejitokeza kuwania nafasi za mwenyekiti , makamo mwenyekiti, katibu mkuu, katibu msaidizi, mweka hazina na wajumbe 6 wa kamati tendaji wenye uwiano sawa wa kijinsia.
Kunambi aliwataja wagombea uenyekiti wa klabu ambao waliidhinishwa pamoja na wagombea wengiine katika kikao cha kamati tendaji ya klabu hiyo kilichofanyika Agosti 3 mwaka huu kuwa ni mwandishi wa habari wa shirika la utangazaji Zanzibar (ZBC) Abdalla Abdulrahman Mfaume na mtangazaji wa shirika hilo Suleiman Abdalla Mohamed, huku nafasi ya umakamo mwenyekiti ikiwaniwa na mwandishi wa star tv na redio free afrika Zanzibar Abdallah Pandu na Rahma Suleiman Ali wa gazeti la Nipashe na redio Chuchu FM.
Wagombea wengine na vituo vyao vya kazi katika mabano ni Faki Mjaka (idara ya habari maelezo Zanzibar) anaewania ukatibu mkuu ambaye hana mpinzani, Takdiri Ali Suwedi (zbc radio ) na Mwinyimvua Abdi Nzukwi (mwandishi wa kujitegemea) wanaochuana katika nafasi ya unaibu katibu wakati nafasi wa mweka hazina ikiwa na mgombea mmoja pekee Halima Tamim Hussein anaetokea chuo cha Mwenge Community Center (MCC).
Katika nafasi nafasi ya mweka hazina msaidizi katibu kunambi alisema haijagombewa na mwanachama yeyote hadi mwisho wa muda uliowekwa kwa ajili ya wanachama hao kuchukua na kurejesha fomu ambao ulikuwa Agosti 3, mwaka huu na kwa upande wa nafasi 3 za wajumbe wa kamti tendaji wanaume, waliojitokeza kugombea nafasi hizo ni Abdalla Pandu (Star TV / radio free afrika), Saleh Hassan ‘Ambrose’ (mwandishi wa kujitegemea), Ishaka Omar (uhuru na mzalendo) , Maulid Kipevu (ZBC TV) na meneja wa Baraza la habari Tanzania MCT ofisi ya Zanzibar, Suleiman Seif Omar.
Kwa upande wa wanawake nafasi hizo zinawaniwa na mjumbe wa sasa wa kamati tendaji Ghania Mohamed, mwandishi wa shirika la magazeti ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wachapishaji wa gazeti hili Mwashamba Juma na mtangazaji wa ZBC redio Aziza Hassan.
Aidha Kunambi aliwawashukuru wagombea hao kwa kujitokeza kwa ajili ya kutumia haki yao ya kikatiba na kuwapongeza wanachama wa klabu hiyo kwa kuonesha hamasa ya kushiriki mkutano huo.
“Kujitokeza kwao japo kulikuwa kwa kusuasua lakini kumetupa faraja sana na bila shaka wao wenyewe wamejipima na sisi tumeridhika kuwa wote wana sifa za kikatibaza kuwawezesha kushika uongozi wa klabu na kuifikisha pale wanachama wengi tunapokutarajia”, alisema katibu huyo.
Mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa EACOTANAL Kikwajuni mjini hapa Zanzibar pamoja na uchaguzi huo pia ambao pia utapokea taarifa za utekelezaji wa klabu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita itakayowasilishwa sambamba na taarifa ya mapato na matumizui ya fedha katika kipindi hicho na kutoa makadirio ya mapato na matumizi ya klabu katika kipindi kijacho.
No comments:
Post a Comment