Habari za Punde

Tarehe za kuhakiki taarifa za wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHAKIKI TAARIFA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Tunawatangazia wananchi wote waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR kujitokeza katika vituo walipojiandikisha ili wahakiki taarifa zao. Ambako daftari la mpiga kura limebandikwa. (Display)  
NA.
MIKOA
TAREHE YA KUANZA
TAREHE YA KUMALIZA
1
Njombe, Iringa,  Mtwara, Lindi, Ruvuma, Katavi, Rukwa, Mbeya, Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Kagera, Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Morogoro.

07/08/2015
11/08/2015
2
Pwani na Zanzibar
11/08/2015
15/08/2015
3
Dar es Salaam
13/08/2015
17/08/2015

Mashine zitakuwa katika OFISI YA AFISA MTENDAJI WA KATA  kwa ajili ya kusahihisha makosa yaliyojitokeza wakati wa kujiandikisha.

 Kwa waliohama wakahamishe taarifa zao ziwepo mahali watakapopigia kura tarehe 25/10/2015
Siku ya UCHAGUZI MKUU.


Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
S.L.P. 10923, Dar es Salaam

Tunza kadi yako, Usimpe Mtu.
JITOKEZE SASA, NENDA KAHAKIKI TAARIFA ZAKO.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.