Habari za Punde

Mgombea Urais wa Chama cha SAU Achukua Fomu ya Urais wa Zanzibar.

Mgombea wa Urais wa Chama cha Sauti ya Umma SAU Ndg Issa Mohammed Zonga akiwasili katika viwanja vya Afisi ya Tume zilioko katika Hoteli ya Bwawani Zanzibar kwa ajili ya kuchukua Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama chake akiwa na wanachama wake 
Mgombea Urais wa Chama cha Sauti ya Umma SAU akiwa na Viongozi wa Chama hicho wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha akitowa maelezo ya fomu ya kugombea Urais akiisoma katika ukumbi wa salama kabla ya kumkabidhi mgombea. 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mhe Jecha Salum Jecha akionesha Mkoba wa Fomu ya Ugombea Urais wa Zanzibar kwa Wananchi waliofika Afisi za Tume kumsindikiza Mgombea Wao kabla ya kumkabidhi Mkoba huo ukiwa na famo za kugombea Urais wa Zanzibar.kushoto Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Mhe Omar Mapuri na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Salum Kassim Ali.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha akimkabidhi Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Mgombea wa Chama cha Sauti ya Umma SAU, Ndg Issa Mohammed Zonga wakati wa hafla hiyo iuliofanyika katika Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma ( SAU ) Ndg Issa Mohammed Zonga akiwa na mkoba wake wa Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar akionesha baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha katika Afisi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ziliko katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar,  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.