Habari za Punde

Mgombea wa Chama cha ADA-TADEA Mhe Juma Ali Khatib Achukua ya Kuwania Urais wa Zanzibar.

 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe. Jecha Salum Jecha akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Fomu ya Urais wa Zanzibar kwa Mgombea wa Chama cha ADA-TADEA Mhe Juma Ali Khatib katika Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hoteli Zanzibar.

Tayari Wagombea Wane wa Urais wa Zanzibar wamejitokeza kuchukua Fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar kupitia Vyama vyao.

Jumla ya Vyama vya Siasa 12 Zanzibar vimepeleka maombi ya Wagombea wao Nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa mwaka huu. Vyama hivyo vilivyojitokeza katika nafasi hiyo

 1.Chama cha Mapinduzi (  CCM,)  
2. Chama cha Wananchi( CUF), 
3. Africa Democratic Alliance Party, (ADA-TADEA )  
4.Alliance For Tanzania Farmers Party (,AFP ), 
5 United People Democratic Party (UPDP) , 
6 Chama cha Ukombozi wa Umma  (CHAUMMA)  
7. Alliance For Democratic Change (,ADC) 
8.Democratic Party (,DP) 
9.Chama cha Demokrasia Makini (,DM ) 
10.Jahazi Asilia (JA) 
11. Alliance For Change and Transparency (ACT-W) na 
12. Sauti ya Umma (SAU) 
Mgombea Urais kupitia Chama cha ADA-TADEA Mhe Juma Ali Khatib akiwa na Viongozi wa Chama hicha wakifuatilia maelezo ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar akizungumza wakati wa kukabidhi kwa fomu ya Urais kwa Mgombea huyo katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Wanachama wa Chama cha ADA-TADEA wakifuatilia maelezo hayo kwa makini kaika ukumbi wa Salama zilioko Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutowa fomu kwa Wagombea wa Urais wa Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe Jecha Salum Jecha akionesha Mkomba wa Fomu ya Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha TADEA kabla ya kumkabidhi wakati wa hafla hiyo ya utoaji wa fomu za Urais wa Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC  Mhe Jecha Salum Jecha akikabidhi kabrasha la Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar Mgombea wa Chama cha ADA-TADEA Mhe Juma Ali Khatib, kugombea nafasi hiyo kupitia Chama chake, hafla hiyo imefanyika Afisi za Tume ya Uchaguzi Ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
  
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia ADA-TADEA Mhe Juma Ali Khatib akiwa na Wananachama wake baada ya kukabidhiwa fomu yake ya kuwania nafasi ya kugombea Urais wa Zanzibar katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Bwawani Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ADA-TADEA Mhe Juma Ali Khatib akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar baada ya kukabidhiwa fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.