Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan na wakilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine akipokewa katika ofisi ndogo ya CCM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam baada ya kutoka Tume ya Uchaguzi kuchukua Fomu za kugombea Urais leo agosti 4, 2015.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk Jakaya Mrisho Kikwete akimlaki Mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Magufuli alipowasili katika Viwanja vya Afisi ya CCM Lumumba Dar mchana huo.
Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mgombea wa Urais wa CCM Dk Magufuli alipowasili viwanja vya CCM Lumumba mchana huo.
Mgombea Mweza wa Urais wa Tanzania Samiha Sululu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika viwanja vya Afisi ya CCM Lumumba baada ya kurejea kuchukua Fomu ya kugombea Urais Tume ya Uchaguzi.
Mgombea Mweza wa Urais wa Tanzania Samiha Sululu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika viwanja vya Afisi ya CCM Lumumba baada ya kurejea kuchukua Fomu ya kugombea Urais Tume ya Uchaguzi.
Katibu Mkuu wa CCM Abdullraham Kinana akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Dar-es-Salaam katika viwanja vya Afisi ya CCM Lumumba wakati wa hafla ya kuchukua fomu ya kugombea Urais Dk John Magufuli na Mgombea wake Mwenza Samiha Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Dar-es-Saalam wakati wa hafla ya kumpokea Mgombea wa CCM akichukua fomu ya kugombea Urais wa Tanzania mkutano huo umefanyika katika Afisi Kuu ya CCM Lumumba Dar.
Mgombea Urais wa Tanzania Dk John Magufuli na Mgombea wake Mwenza Samiha Suluhu Hassan wakipanda katika jukwaa kusalimiana na Wananchi na kuonesha fomu yake ya kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM.

Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania Samiha Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Dar-es-Salaam wakati wa kurejea kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM.
Tunampenda Magufuli, lakini tunavyoichukia ccm kama ukimwi, sijui kama utapata kura yangu. Samahani sana
ReplyDeleteAh, mimi nalia na mzee wangu wa 'umbuji' naona mwaka huu kura zake hazikutosha ktk jimbo la uzini sijui hata alikosea wapi au ndio tuseme majukumu ya NEC yalimzidia!
ReplyDeleteHata hivyo nadhani kutokana na uzoefu alionao kwenye siasa na kwa namna Magfuli anavyomuangalia hapa anaweza akamkumbuka!
Ukweli ni kwamba Magufuli sio mwanasiasa mzoefu bali ni mtendaji zaidi na hasa kwa upande wa siasa za Z'bar ambazo zinataka 'matao' sina shaka Dr. Moh'd seif Khatib atamsaidia pindipo atataka msaada wake! Vinginevyo ataendelea kumwaga 'lectures za Kiswahili" pale UDOM.