SHEHA wa shehia ya Mtambile wilaya ya
Mkoani Pemba, Rajab Zaid Risasi, akizungumza kwenye mkutano wa wazi juu ya
kutoa msaada wa kisheria, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar
ZLSC tawi la Pemba, kulia ni Afisa Mipango wa kituo hicho Siti Habib Salum,
akifuatiwa na Mratibu wake Fatma Khamis Hemed, mwanasheria kutoka afisi ya
Mkurugenzi wa mashitaka Seif Mohamed Khamis na hakimu wa mahakama ya ardhi
Salum Hassan Bakar, (Picha na Haji
Nassor, Pemba)
HAKIMU wa mahakama ya ardhi mkoa wa kusini Pemba
Salum Hassan Bakari, akimpa masaada wa kisheria mwananchi mmoja wa shehia ya
Mtambile wilaya ya Mkoani, wakati watendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, walipofika hapo kutoa masaada wa kisheria bila ya malipo,
(Picha na Haji Nassor, Pemba).
WANANCHI wa shehia ya Mtambile wilaya ya Mkoani Pemba,
waliohudhuria kwenye mkutano wa wazi wa kutoa msaada wa kisheria bila ya
malipo, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba,
(Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria
Zanzibar, ZLSC Khalfan Amour Mohamed, akigawa majarida kwa wananchi wa shehia
ya Mtambile wilaya ya mkoani Pemba, yaliochapishwa na ZLSC, wakati wa mkutano
wa wazi wa kutoa msaada wa kisheria, (Picha
na Haji Nassor, Pemba)
No comments:
Post a Comment