Habari za Punde

Timu ya Tekeleza yashinda tena, yaiadhibu Al Mapinduzi 2-1

Na Haji Nassor, Pemba
TIMU ya Tekeleza inaendelea kuwatekelezea ahadi wapenzi na washabiki kuhama ligi daraja la pili wilaya, na kuhamia daraja la pili taifa Pemba, baada ya jana tena kuiadhibu timu ya Al-mapinduzi kwa magoli 2-1.
Katika mchezo huo wa sita bora mkoa wa kusini Pemba, ambao unasaka timu tatu zitakazocheza ligi daraja la pili taifa Pemba, ulichezwa uwanja wa Gombani, ambapo washindi walikuwa wa kwanza kujipatia goli.
Goli la kuongozwa lilipachikwa wavuni na Yussuf Mohamed dakika ya 24, huku goli la pili likifungwa na Wahid Mbarouk kunako dakika ya 76, ambapo goli pekee la Al-mapinduzi lilifungwa Hamad Ali dakika 47.
Na katika mchezo mwengine uliochezwa uwanja wa Makombeni majira ya saa 10:00 jioni, timu ya Baruti imepunguzwa kasi baada ya kuchapana goli 1-1 na New star.

Kwa matokeo hayo, timu ya Tekeleza inaendelea kuongoza michauano hiyo, kwa kuwa na alama saba, Baruti tano, Al-mapinduzi nne, Msumari tatu, Datisho na New star zikisota na alama moja moja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.