Habari za Punde

Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Wafanyiwa Tafrija ya Kuwakaribisha Kijiji cha Makumbusho Dar.

Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akiwashukuru wadau mbalimbali ambao  wamefanikisha mchakato mzima wa kuendesha shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Pia Kipekee Amewashukuru wafanyakazi wa Oxfam akiwepo Eluka Kibona na Suhaila Thawer kwa kuwa Mstari wa mbele kufanikisha Shindano hili na Mwisho kuwatakia kila Laheri washiriki wote wanaokwenda katika kushindana kumpata Mama Shujaa wa Chakula.
Baadhi ya washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Sherehe ya kukaribishwa jana katika Kijiji cha Makumbusho.
 Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster wa kwanza kulia akibadilishana mawazo na baadhi ya akina mama ambao watakuwa wenyeji wa wageni washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015

Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea kwa ufupi juu ya Mchakato mzima wa Shindano la Mama shujaa wa chakula ambalo linalenga kuwawezesha wakina mama kutambulika katika kilimo na kueleza Matakwa yao juu ya kilimo endelevu.
Burudani ikiwa inaendelea wakati wa Sherehe za Kuwakaribisha na kuwatambulisha Rasmi Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo limeanza rasmi katika kijiji cha Kasanga wilayani Kisarawe


 Bw. Godia Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasanga akiwakaribisha Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano Linaloendeshwa na Oxfam Tanzania kupitia Kampeni ya Grow Kijijini kwake.
  Bi. Mwanaidi Hamza ambaye anatoka katika Programu ya Big Result now akitoa ushuhuda jinsi gani alivyofanikiwa kulingana na Proramu hiyo na sasa anamaisha mazuri, na kuwasihi wakina mama wasikate tamaa katika kilimo.
Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Jackson Samwel akiwapongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kuanzisha shindano la Mama shujaa wa Chakula , kwa kutambua umuhimu wa ardhi katika kuzalisha chakula, ameshauri akinamama wabadilishane uzoefu pindi watakapokuwa kambini ili kuja na mbinu mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Stephen Mfuko aka Zero akitaja namba za washiriki na Jinsi ambavyo wanaweza Pigiwa Kura  ambapo Programu mzima itaoneshwa katika Runinga ya ITV kila Siku kuanzia Tarehe 2.08.2015-21.08.2015 kuanzia saa 12 Jioni.
 Baadhi ya washiriki wengine wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakifurahia jambo katika Sherehe hizo.
 Baadhi ya Wageni waalikwa Pamoja na Washiriki  wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula linaloandaliwa na Oxfam kupitia Programu ya Grow wakiwa katika sherehe za kuwakaribisha na kuwatambulisha washiriki hao
Mmoja wa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Akijitambulisha..
Mmoja wa Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula aliye vaa Tshirt nyeupe(wa pili kulia) ambalo litaanza kuruka kupitia Runinga ya ITV Kila siku kuanzia 2.08.2015 -21.08.2015 saa 12 Jioni akicheza ngoma ya kwao wakati wakitambulishwa
 Wakina Mama ambao ni Washiriki wa shindano la Kumsaka Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwa wanasema ile 'Slogan' yao ya "Mimi Mama, Najiamini, ewe mama Jitume Pamoja Tunaweza" 
 Baadhi ya akina Mama ambao ndio watakuwa wenyeji wa washiriki wa shindano la Kumsaka Mama Shujaa wa chakula 2015 ambalo linaandaliwa na Oxfam chini ya Kampeni ya Grow.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.