Habari za Punde

Waziri Mkuu mstaafu Sumaye ajitoa rasmi CCM, ajiunga na UKAWA




 Waziri Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kushoto), akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo mchana.
 Waziri Mkuu mstaafu, Fredreck Sumaye (kulia), akipeana mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe Dar es Salaam leo mchana, baada ya kujiunga na chama hicho. Anayeshuhudia katikati ni Mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
 Sumaye akisisitiza jambo
Sumaye (wa tatu kulia), akiwa na viongozi wanaunda Umoja wa Katiba (UKAWA) baada ya kuondoka CCM na kujiunga na Chadema.

CHAMA Cha Mapinduzi, CCM, kimetikiswa tena leo Agosti 22, 2015, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu Mhe. Frederick Sumaye kujivua uanachana na kujiunga na NCCR-Mageuzi, moja ya chama kati ya vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).


Akitangaza uamuzi wake huo moja kwa moja "LIVE" kupitia runinga ya ITV katika jioni ya leo mbele ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jioni hii pale Bahari Beach Hotel, jijini Dar es Salaam, Sumaye amesema, CCM imejaa kiburi.


Amesema kwa kudhihirisha hilo, wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi, viongozi wa chama hichowaliokuwa wakizunguka nchi nzima walijielekeza zaidi kuishambulia serikali badala ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura. 
"Sitoki CCM labda nina hasira na CCM, au sikuchaguliwa kwa vile sikuteuliwa, na wala sitoki CCM ili kudhoofisha Chama cha Mapinduzi, badala yake nakiimarisha."
Sumaye anakuwa Waziri Mkuu mstaafu wa pili kuhama chama tawala, CCM, kama alivyofanya Edward Lowassa, ambaye naye alitangaza kujiunga CHADEMA mwezi Julai baada ya kutokuridhishwa na mchujo wa kupata mgombea Urais wa Tanzania 2015 na kufanikiwa kuteuliwa na chama chake kipya kuwakilisha vyama vinne katika kiti hicho.

Sumaye amesema kuwa, "kulizuia wimbi la mageuzi ninaloliona ni ngumu kweli kweli" na kuwahimiza waliobaki CCM na walio kwenye madaraka, wajiunge na upinzani ili kuharakisha mabadiliko hayo.


1 comment:

  1. Kwakweli hali bado si shwari ndani ya ccm lkn. naamini dhahabu ili iwe dhahabu lazma ipitie kwenye moto, na ccm ili irejee uimara wake wa zamani lazma ipate misuko suko kama hii.

    Tulijiamini kupita kiasi na hii iliwafanya baadhi ya viongozi na wanachama kuwa na kiburi hata pale unapowashauri mambo ya msingi au yanayohatarisha uimara wa chama.

    Leo hii hali imekua 'tete' hata wale wasiotaka kusikiliza ushauri wameshtuka na hawajui la kufanya wamebaki kujiuliza tu... "jamani mbona hivi, tutatoka kweli?"

    Pamoja na kua misukosuko hii ya ccm inatokea zaidi bara lkn. ni wazi kwamba adhari zake zinatukumba moja kwa moja ccm-z'bar

    Hapa kwetu imekua kujitia kwenye ccm ni njia tu ya kutafuta madara na ajira za watoto wetu lkn. sio vinginevyo, tumekua wazembe, viongozi wetu wameshindwa kutafuta wanachama wapya kutoka ktk upinzani badala yake wapinzani ndio wanachukua kutoka kwetu, mfano mansuri na mzee Moyo!

    Ukiwauliza wanakwambi " wache waende" wanajua sasa ulaji utabaki kwao, kampeni zao hazivutii wanachama wapya kutoka upande mwengine ni familia zili zile wanazoziita ccm.

    Ssa wakati umefika wa kuacha" kutumai cha ndugu", wenzetu nao wana hali mbaya lzma na sisi huku tujiimarishe, ule utamaduni wa kusema "wao wao na sisi sisi" tuache lazma tutafute wanacha wapya. naamini baada ya msukosuko huu, tutaelewana vizuri, nani ccm- damu na nani maslahi!


    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.