Habari za Punde

ZLSC tawi la Pemba watoa msaada wa sheria bila ya malipo Micheweni Pemba

  SHEHA wa shehia ya Mlindo wilaya ya Micheweni Pemba, Said Salim Issa akifungua mkutano wa wazi, kwa wananchi wake na shehia yengine, ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, juu ya kutoa msaada wa kisheria bila ya malipo, ambapo ZLSC iliambatana na wanasheria mbali mbali, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
  WANANCHI wa shehia ya Mlindo wilaya ya Micheweni Pemba, wakimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed, akielezea lengo la mkutano wa wazi wa kutoa msaada wa kisheria bila ya malipo kwa wananchi wa wilaya ya Micheweni, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Safia Saleh Sultan, akimpa msaada wa kisheria mwananchi mmoja wa shehia ya Mlindo wilaya ya Micheweni Pemba, wakati watendaji wa ZLSC na wanasheria wengine, walipofika shehiani hapo kutoa msaada huo bila ya malipo, (Picha na Haji Nassor, Pemba).  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.