Mgombea wa Jahazi Asilia Ndg Kassim Ali Bakari akiwasili katika viwanja vya Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko katika hotli ya bwawani Zanzibar kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Jahazi Asilia Ndg Kassim Ali Bakari akiwa na viongozi wa Chama hicho wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) akisoma maelezo ya fomu ya kugombea Urais wakati wa hafla hiyo bwawani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Salum Kassim Ali akitowa maelezo ya mgombea kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kumkabidhi Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)Mhe Jecha S Jecha akionesha mkoba wenye fomu za Urais wa Urais wa Zanzibar kabla ya kumkabidhi Mgombea wa Chama cha Jahazi Asilia.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha S Jecha akimkabidhi mkoba wenye fomu za kugombea Urais wa Zanzibar mgombea wa Chama cha Jahazi Asilia Ndg Kassim Ali Bakari, wakati alipofika tumu kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais kupitia cha cha Jahazi Asilia Ndg Kassim Ali Bakari akionesha mkoba wake aliokabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ukiwa na Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar. akiwa katika ukumbi wa salama bwawani Zanzibar.
Mgombea Urais kupitia Chama cha Jahazi Asilia Ndg Kassim Ali Bakari akizungumza baada ya kukabidhiwa fomu ya Urais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mhe Jecha S Jecha katika afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko katoka ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibae
No comments:
Post a Comment