Na Abubakar Kisandu, Zanzibar
Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kimethibitisha kupokea barua nyingine kutoka shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) ambayo yenye kichwa cha habari kinachosema “YAH: SUALA LILILO MAHAKAMANI DHIDI YA ZFA”.
Barua hiyo ambayo imetoka kwa katibu mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine na kutumwa kwa katibu mkuu wa ZFA Kassim Haji Salum.
Katika barua hiyo ambayo ilijikita zaidi kwa mambo ya soka kupelekwa mahakamani ambapo ikielezea kusitishwa kwa kozi ya ukocha ya leseni B ambayo imesitishwa, pia ikisitisha kozi nyingine zinazoendeshwa na TFF, CAF na FIFA.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa na huzuni ya hali ya juu kwenye mtandao huu, makamo wa Urais wa ZFA Pemba Ali Mohammed amesema kuna watu wanajiita wadau wa michezo Zanzibar wanaotaka mabadiliko lakini wao ndo wana haribu soka na kuvishawishi vilabu kwenda mahakamani.
Athari nyingine ambazo huenda kujitokeza kwa soka la Zanzibar kwasasa ni kama zifu atazo.
Waamuzi wa Zanzibar kwenye kopa test kule bara hawatokwenda tena, lakini pia wale waamuzi wenye beji ya FIFA ambapo sasa hivi wengine wapo nje ya nchi kusimamia michezo ya kimataifa mfano Mgaza Ali Kinduli na Waziri Sheha wapo Sudan ambapo pengine wakirejea Zanzibar na wao wataathirika.
Timu ya taifa Zanzibar (Zanzibar Heroes) nao huenda wakakosa kushiriki michuano ya Challenge Cup, mashindano ya vijana ya Copa Coca-cola kwa mikoa ya Zanzibar haitoshiriki tena.
Kombe la Mapinduzi vilabu vya Tanzania bara na nje ya Tanzania pia havitotia mguu hapa visiwani na pia vilabu vya Zanzibar, bingwa na makamu bingwa Mafunzo na JKU ambao watawakilisha kwenye klabu bingwa barani Afrika na Kombe la shirikisho pengine na wao wasishiriki tena kwasababu ya figisufigisu za soka kupelekana mahakamani.
No comments:
Post a Comment