Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni wakati alipowasili kuzungumza nao.
Balozi Seif akizungumza na Wananchi na Wana CCM wa Kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni akitekeleza ahadi aliyotoa kwa Wazee Waasisi wa Kijiji hicho ya kufika kusalimiana nao.
Balozi Seif akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akiagana na Wana CCM wa Kijiji cha Kwale mara baada ya kuzungumza nao katika Mkutano wa hadhara
.(Picha na –OMPR –ZNZ).
Na Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewatahadharisha Wananchi kuwa makini na Watu wanaochochea chuki miongoni mwa Jamii jambo ambalo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kamwe haitakubali kuona amani ya Nchi inachezewa kizembe.
Alisema wapo watu waliochoka na amani iliyopo nchini kwa kuanza kushabikia cheche za kujiandaa kuwashawishi Vijana wawe tayari kufanya fujo mara tuu baada ya zoezi la kupiga kura kwenya uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.
Balozi Seif Ali Iddi ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na Wananchi amoja na Wana CCM wa Kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba akitekeleza ahadi aliyowapa wazee wa Kijiji hicho hivi karibuni ya kuwatembelea na kusalimiana nao.
Balozi Seif aliwaonya Vijana kujiepuka na mtego huo ulioandaliwa kwa ajili yao unaoweza kuwaathiri na akawatolea mfano wa matukio ya Januari mwaka 2001 ambayo waandaji wakubwa waliwazuia Vijana wao na kuwaachia Vijana wa wenzao kutumbukia katika balaa.
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika siku 49 zijazo Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM aliwakumbusha wana CCM na Wananachi hao wa Kijiji cha Kwale kuendelea kuiunga mkono CCM ibakie madarakani.
Alisema Dira ya Cahama cha Mapinduzi ni kuwanuganisha Wananachi wote katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwani tabia ya mfarakano inayoonekana kubebwa na upinzani imepigwa vita hata katika vitabu wa Dini.
Balozi Seif amewapa pole Wananchi wa Kijiji hicho cha Kwale kutokana na madhila waliyoyapata kufuatia kitendo cha Upinzani kutaka kupachika Bendera kwa nguvu ndani ya Kijiji hicho bila ya ridhaa ya Wananchi wenyewe.
Alisema Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kamwe hawakubali kuonewa na Uongozi wa Chama hicho katika ngazi zote daima utaendelea kutetea maslahi yake muda wowote ule.
Katika Mkutano huo Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kuizindua rasmi Maskani ya Chama cha Mapinduzi ya Wazede wa Kijiji hicho cha Kwale kiliomo ndani ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
No comments:
Post a Comment