Habari za Punde

Kalamu za waandishi zisichukue mamlaka ya visanduku vya kura


-Kufuata maadili, miiko, sheria ndio uandishi wa habari
Na Haji Nassor, Pemba
KUMEKUCHA Tanzania vyama vya siasa vinahaha kila kona ya nchi kuhakikisha mwisho wa siku wanaibuka na ushindi kwenye uchaguzi mkuu wa vyama vingi.
Ni harakati za kisiasa, zinazoelezwa kuimarisha demokrasia ya kila baada ya miaka mitano, kwa wananchi kuvisogelea tena visanduku vya kura.
Ni sawa na kwamba wananchi kila miaka mitani huulizwa kwa njia ya kupiga kura iwapo wanabakia na viongozi wao wa zamani ua wanataka kuwabadilisha.
Ndio maana kila chama hujifungia kwenye vikao vizito kuhakikisha mwishi wa siku wanaibuka na mgombea mwenye sifa zote ili aingia kwenye ushindani.
Tanzania pamoja na kuwa na vyama 22 ya siasa, huwa sio vyama vyote vyenye uwezo wa kusimamisha hata wabunge, wawakilishi, madiwani na rais.
Lakini kwa vyama vilivyosimamisha wagombea kwa ngazi mbali mbali, huwa na dira, sera, ilani na mitazamo yao ambayo huyauza kwa wapigara kura.
Waandishi wa habari huwasambamba na wagombea hao kuandika habari zao na kutengeneza vipindi mbali mbali, na wengine wakisahau kufuata maadili yao.
Wapo waandishi wamekuwa wakiwahukumu wagombea kwa kuwaita ni wagombe kutoka vyama vidogo, ingawa kwa msajili wa vyama hili halipo.

Wanaotengeza vipindi ya tv au redio huwawapi kipaumbele wagombea wa vyama vyengine, kwa AFP, ACT, DP, TLP, UDP, SAU, UPDP, NRA, PPT-Maendeleo au CHAUSTA wakidai haivia wafuasi wengi.
Sasa hapa waandishi ni kuvihukumu vyama hivi nje ya kisanduka cha kura jambo ni kuvunja miiko na maadili ya kazi ya uandishi wa habari.
Yapo maadili kadhaa kama vile mezania ‘balance’ kwa waandishi ambapo hutakiwa kutoa haki sawa iwe ni kwenye kutengeneza vipindi au kuandika habari za kawaida.
Mwandishi wa habari wa siku nyingi Ali Uki, wakati akiwaidhi waandishi wa habari wa Zanzibar kwenye mafunzo yalioandaliwa na MCT kwa kushirikiana na BBC, anasema kufuata maadili ndio jambo la kwanza.
“Wapo waandishi wa habari wamekuwa wakivikuhumu baadhi ya vyama, kwa kuiviita vidogo, havina wafusi wengie, kumbe kazi hiyo ilipaswa ionekane wakati wa kupiga kura’’,alisema.
Uki anasikitishwa na baadhi ya waandishi wa habari na vyombo vyao kalamu zao kuzitumia kwa mitazamao yao badala ya kufuata maadili na sheria zao.
“Wala mwandishi hajikuti kwenye mazingira magumu iwapo ataamua kutoa mezania iliosawa kwa wagombea wa vyama vyote’’,alisema.
Ingawa aligusa hasa vyombo vya Umma kama vile ZBC, TBC, gazeti la Habari na Zanzibar leo, kwamba has ahivi havina jinsi wala namna nyengine bali ni kuwatendea haki wagombea wote.
Lakini akatahadharisha kuwa hata vyombo vyengine vya binafsi vinajukumu la kuhakikisha pale wanamuandikia mgombea wa chama Fulani, basi wasibakishe chembe ya masuali kwa wasikilizaji au wasomaji.
Hili liliungwa nguvu na Mejena wa MCT ofisi ya Zanzibar Suleiman Seif Omar, kwamba suala la kutumia kalamu vyema kwa waandishi wa habari ndio jambo la kwanza.
“Mafunzo munayoendelea kupewa na MCT na taasisi nyengine lengo hasa ni kuhakikisha hakuna chama kitakachoonewa katika upashanaji wa habari kuelekea uchaguzi mkuu’’,alifafanua.
Mwandishi wa habari wa siku nyingi Zanzibar Shifaa Said yeye anasema kama maadili ya kihabari yamefahamika vyema hakuna jana kwa waandishi wa habari kufanya kazi ya kundi jengine.
“Kazi ya nani mshindi, nani hana wafuasi wengi itathibitishwa na wananchi wenyewe kwenye kisanduku cha kura sio waandishi kujibebesha mabango ya uhakimu’’,alisema.
Alitaja maadili kama ya kutopokea rushwa, kwamba iwapo waandishi watapokea wasitarajie kuandika habari yenye kiwango na badala yake ni kuijiingiza kwenye ushabiki.
Jengine alilolipigia kelele ni kuacha kupanda gari za wagombea, anasema hilo ni aina nyengine ta rushwa ambayo wapo waandishi wengine hilo wamekuwa wakilifanya.
Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Zanzibar Tali Ussi Hamad, yeye anathibitisha kuwa wapo waandishi wa habari wamekuwa wakichukua nafasi ya Tume ya uchaguzi kw akutoa matokea kabla.
“Mwandishi kwa utashi wake, anaweza kuandika habari ikawa na dalili ya kumbeba mgombea wa chama anachotaka yeye, kwamba ameshinda wakati suala la kutangaaza hayo ni tume yenyewe’’,alifafanua.
Waandishi wa habari tayari wapo  hivi sasa kuelekea uchaguzi mkuu ambao wameshapiga mbeleko wagombea, na kuanza kuwapa matope wengine.
Baada ya hapo kinachofuata ambacho hufanywa na baadhi ya waandishi wa habari, ni kuwaamulia wananchi kwamba mgombea wa chama X hafai.
Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar no 11 ya mwaka 1984, ukiangalia kifungu cha 39 kuanzia (1-3) kimetoa mamlaka kwa mwananchi kupiga kura, lengo ni kumchagua mgombea amtakae.
Haki ya kupiga kura ilianza kwenye katiba zetu, maana Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwenye Ibara ya 5, huku ile ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 7, vimeeleza suala la haki ya kupiga kura.
Sasa iweje vyombo vya habari kupitia kalamu zao ziwe mithili ya visanduku vya kupigia kura, kwa kuwachagulia wananchi mgombea?
Suala la maamuzi juu ya aina gani ya mgombea, bado litabakia mikononi mwa wananchi wenyewe, na kazi ya kuelimisha na kuchambua itabaki kwa wandishi wa habari.
Lilian Timbuka kutoka gazeti la Mwananchi, anasema kwa nji moja lazima wahariri wawajibike ipasavyo wanapopokea bahari za waandishi wao.
Lengo ni kuhakikisha iwapo mwandishi wameshakua rushwa kwa lengo la kumchafua mgombea wa chama chengine, waweze kuligundua kupitia uandishi wake.
“Wakati mwengine muhariri alie mahari lazima anaweza kuibua madudu ya kihabari yanayofanywa na mwandishi wake, yenye ishara ya kuwachagulia mgombea wananchi’’,alisema.
Hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari jiji Mbeya, katika semina ya kuandika habari za uchaguzi Naibu Mkurugenzi Idara ya utangazaji TCRA makao makuu, Fredrick Ntobi amewasisitiza waandishi wa habari,  kuhakikisha wanafuata maadili ya kazi zao.
Ntobi hakuacha kusema,  ili kuepuka madhara yatakayoweza kujitokeza pindi watakapotoa taarifa potofu kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu na chaguzi nyingine zitakazofuata, ni vyema jukumu la kuchagua mgombea walibakishe kwa wananchi.
Mkuu wa taalumu kutoka chuo cha uandishi wa habari Zanzibar ZJMMC, Rashid Kombo Omar, akiwa katika mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za uchaguzi, anasema ujenzi wa demokrasia ya kweli kupitia mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi unahitaji kwa kiasi kikubwa mchango wa vyombo vya habari.
Lakini akatahadharisha kuwa mchango ambao ameutaka kuwa ni makini, ulenge zaidi katika kuisaidia jamii kuchagua viongozi wanaofaa na wanaomudu kuchapuza kasi ya maendeleo wanayoyahitaji.
“Isiwe vyombo vya habari vinajipa mamlaka ya kuwachagulia wananchi viongozi, na kujifafanisha kama wao ndio visanduku vya kura na kuvaa joho la Tume za uchaguzi huko ni kukiuka maadili ya kazi zao’’,alisema.
Kama vyama vya siasa ziaid ya 20 vimesaini "Maadili ya Uchaguzi" yatakayotumika wakati wa kampeni, kupiga kura na wakati wa kutangaza matokeo, sasa iweje kwa waandishi wayakiuke ya kwao.

Tena zuri zaidi mwenyekitu wa Tume ya taifa ya Uchaguzi NEC, Jaji Lubuva alisema Maadili yanapaswa kuanza kutumika rasmi Agosti 22 mwaka huu wakati kampeni za uchaguzi zitakapoanza, ingawa kwa wanahabari naamini ya kwao ni yakudumu.


Kufuata maadili ya kiuwandishi na sheria zake, haswa ndio unaoitwa uwandishi uliotukuka, na kinyume chake ni ukanjaja uliobobea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.